Saturday, January 19, 2013

YANGA YAICHAPA BLACK LEOPARD YA BONDENI 3-2!


kabange twite akichuana na mchezaji wa black leopards


WIMBI LA TEGETE KUCHEKA NA NYAVU LAMPA JINA “MTURUKI!”

Vinara wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga, ambao pia ndio Mabingwa wa Soka Afrika Mashariki na Kati, leo wakicheza Mechi yao ya kwanza tangu warejee kutoka Antalya, Uturuki waliko piga Kambi ya Mazoezi ya Wiki mbili, wameichapa Black Leopard ya Afrika Kusini Bao 3-2 katika Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.


hawa ni mashabiki wa yanga

MAGOLI:
Yanga 3
-Tegete Dakika ya  32 & 73
-Domayo 63
Black Leopard 2
-Khoza Dakika ya 47
-Rodney  89 

Nyota wa Mechi hii alikuwa Jerry Teget aliefungia Yanga Bao 2 akiendeleza wimbi la kufunga aliloanza huko Uturuki kati Mechi za kujipima nguvu kiasi ambacho Washabiki wa Yanga wameanza kumpachika Jina ‘Mturuki!’.

KIKOSI cha YANGA:
1.Ally Mustafa 'Barthez'
2.Mbuyu Twite
3.Oscar Joshua
4.Nadir Haroub 'Cannavaro'
5.Kelvin Yondani
6.Athumani Idd 'Chuji'
7.Kabange Twite
8.Frank Domayo
9.Didier Kavumbagu
10.Jerson Tegete
11.Haruna Niyonzima
Akiba:
1.Said Mohamed
2.Godfrey Taita
3.Stephano Mwasika
4.Ladislaus Mbogo
5.Shadrack Nsajigwa
6.Nurdin Bakari
7.Saimon Msuva
8.Omega Seme
9.Said Bahanuzi
10.George Banda
11.David Luhende
12.Rehani Kibingu
13.Nizar Khalfani
14.Juma Abdul

No comments:

Post a Comment