Sunday, May 5, 2013

HIKI NDICHO WALICHOKISEMA MKUU WA MKOA WA ARUSHA, RPC NA Mh. LEMA BAADA YA KUFIKA KWENYE KANISA LILILOLIPULIWA KWA BOMU...!


DSCN2227 
Hali ya eneo mlipuko ulipotokea
DSCN2220 
Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea
DSCN2228 
Ulinzi umeimarishwa
DSCN2252
DSCN2246 
Wanasualama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio
DSCN2282
DSCN2258 
Magesa Mulongo akiteta na RCO wa Mkoa wa Arusha
DSCN2273 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na wananchi kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa. Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
DSCN2236 
Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia. Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi.
DSCN2251
DSCN2267 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri wa Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo.
DSCN2276
DSCN2255
DSCN2281

DSCN2222
DSCN2215
DSCN2218
DSCN2219 


Godbless Lema ambaye ni mbunge wa Arusha na ametembelea eneo la kanisa lililolipuliwa na bomu na kuwafariji wahanga wa tukio hilo. Akiongea kwa jazba na hasira na wananchi waliopo eneo la tukio, Lema ameitumu serikali kwa mara nyingine na kudai kuwa uzembe wa viongozi ndo chanzo cha matukio kama haya.

Hotuba fupi na nasaha zake zilikuwa zikisikika moja kwa moja kupitia Radio maria kabla ya kituo hicho kuamua kukatisha nasaha zake. Haijafahamika mara moja sababu za kukatishwa kwa hotuba yake.
 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mulongo alifika  eneo ambalo ndio kanisa la katoliki lililolipuliwa na bomu lilipo na kuwafariji wahanga wa tukio la bomu.

RPC wa mkoa wa Arusha naye aliambatana na mkuu wa mkoa na  alikuwa anatoa nasaha zake kwa wananchi. RPC ameeleza kuwa tukio hili ni la kigaidi. Katika maelezo yake, RPC amesema kuwa aliyehusika alijitokeza nyuma ya jengo kwa kujificha na kurusha bomu.

Amesema Polisi wanawasaka waliohusika na unyama huu na ameomba yeyote mwenye taarifa yoyote aisaidie polis. 



Waliojeruhiwa mpaka sasa ambao wapo katika hospitali ya mkoa  ya MOUNT MERU ni 42 .huku mmoja akiwa amefariki kutokana na mlipuko huo na alitambulika kwa jina la REGINA LONING’O KURESOI mkazi wa ORASITY JIJINI ARUSHA.



Kwa taarifa ambazo mjukuu wa tozo imezipata ni kwamba Mpaka sasa  mtu mmoja anashikiliwa  na  polisi kwa mahojiano  zaidi