Sunday, February 24, 2013

MURUSAGAMBA HATARINI KUKUMBWA NA NJAA



NGARA
Wakazi wa kijiji cha Murubanga kata ya Murusagamba wilayani Ngara huenda wakakumbwa na baa la njaa kutokana na kundi la tembo kushambulia zaidi ya ekari 60 za mahindi kijijini humo

Diwani wa kata ya Murusagamba Bw Soud Mkubila amesema kuwa tembo wanaokadiriwa kufikia 50 wamevamia eneo la Mulonzi yaliko mashamba mengi ya wakazi wa kijiji cha Murubanga

Amesema taarifa kuhusu uharibifu huo zimetolewa kwa halmashauri ya wilaya ya Ngara ili wataalamu wende kuwafukuza tembo hao waliovamia kijijini humo tangu juzi na kusababisha hofu kwa wanakijiji

Bw Mkubila amesema kuwa wataalam wa idara ya wanyamapori kutoka halmashauri ya wilaya ya Ngara wamekwenda kijijini humo leo kwa ajili ya kuwafukuza tembo hao na kufanya tathmini ya uharibifu uliojitokeza

Wzazi wanaoshindwa kupeleka watoto shule kukamatwa-Ngara


Na. Mrisho Salum
NgaraSerikali wilayani ngara imeanza zoezi la kuwakamata wazazi ambao hawajawpeleka shule wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari kwa ajili ya chukuliwa hatua za kisheria.
 
Akizungumza na mwandishi wa habari hii ofisini kwake kaimu katibu tawala wa wilaya ya Ngara david mafipa amesema zoezi hilo litaanza katika kata za murukulazo,ntobeye na kumalizia kata ya kanazi.
 
Bw.Mafipa amesema kuwa asilimia 40 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu hawajaripoti katika shule walizopangiwa.
 
Alinukuliwa akisema
"TUTAWAKAMATA KAMA TULIVYO AHIDI NA TUWAPELEKA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA WAKAJIBU MASHTAKA,KAMA TULIVYOSEMA KWAMBA TUTAAKIKISHA HAKI ZA WATOTO WANAPATA IKIWEMO HAKI YA ELIMU NI WAJIBU WA MZAZI KUAKIKISHA MWANAE ANAKWENDA SHULE"
 
Aidha amesema zoezi hilo ni endelevu na litafanyika kwa wilaya nzima ili kuwabaini wazazi ambao wameshindwa kuwapeleka watoto wao shule kutokana na visingizio mbalimbali ili wafikishwe katika vyombo vya sheria
 
Kwa upande wao wananchi walikipongeza kitendo cha serikali wilayani ngara kuwachukulia hatua wazazi ambao hawajawpeleka shule watoto wao waliochaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari nakuiomba serikali ijizatiti kwa zoezi hilo kutokana na zoezi hilo kuwa gumu.
 
Mmoja ya wananchi Bw.Goerge Andrew alisema kuwa serikali inatakiwa kujizatiti vilivyo kwa ajili ya zoezi hilo
"Kiukweli serikali yetu imefanya jambo zuri kutokana na umuhimu wa elimu kwa watoto kwa sasa ila inatakiwa ijizatiti kutokana na wazazi wengine wasioelewa kuwaficha watoto ama kukimbia"

WALIMU WATAKIWA KUTAMBUA WAJIBU WAO



Na James jovin
KIBONDO
Paroko Christopher Ndizeye wa parokia ya Kibondo mkoani Kigoma amewataka walimu kutambua kuwa ualimu ni wito hivyo wanatakiwa kuifanya kazi hiyo kwa moyo na uzalendo ili kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi

Padre Ndizeye amesema hayo juzi  alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya tisa ya kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wasichana Bon Konsil wilayani Kibondo

Amesema iwapo walimu watafanya kazi zao kwa moyo wa dhati na kuweka uzalendo mbele watasaidia wanafunzi kupenda masomo hali itakayoinua kiwango cha taaluma nchini


Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Sister Generoza Mpilirwe ametoa wito kwa serikali kutafuta kiini cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu kila mwaka na kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo

Kiongozi wa NCCR MAGEUZI ASIMAMISHWA





Na Mrisho Salum-NGARA

Chama cha NCCR-Mageuzi mkoani Kagera kimemsimamisha mwenyekiti wa chama hicho wilayani Ngara Bw Kennedy Stanford Festo kwa kukiuka katiba ya chama chake na kushiriki maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM

Kamishna wa chama hicho mkoani Kagera Bw Peterson Mushenyera amesema kuwa uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha kamati tendaji ya chama hicho wilaya ya Ngara kilichofanyika juzi

Amesema kuwa Bw Festo amesimamishwa kwa muda wa siku 14 kutokana na kuvunja katiba ya chama chake na kuhudhuria maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika February 5 katika kata ya Kabanga wilayani Ngara

Bw Mushenyera amesema kuwa Bw Festo pia ameandikiwa barua ya kujieleza kwa kamati ya nidhamu ya chama hicho wilayani Ngara inayoongozwa na mwenyekiti Wyclif Samwel

Amenukuliwa akisema “Ninasema tunamsimamisha uenyekiti mpaka kesi yake itakapo kwisha na chama chetu hakina ushirikiano na chama cha mapinduzi


Aidha kamati hiyo ya utendaji ya NCCR-Mageuzi wilayani Ngara imemteua Bw Joseph Bucha kukaimu nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho wilayani Ngara katika kipindi alichosimamishwa Bw Festo

Wapanda pikipiki marufuku kupakia abiria zaidi ya mmoja




Mrisho Salum
Ngara-kagera
Katibu wa chama cha wapanda pikipiki wilayani Ngara Bw Castory Paschal amewataka wapanda pikipiki wilayani humo kujenga kawaida ya kutii sheria bila shuruti ili kuepuka mikwaruzano na vyombo vya sheria na kuepuka ajali zinazoweza kuepukika

Akizungumza na mjukuu wa tozo Bw Paschal amesema kuwa wapanda pikipiki wengi wilayani humo hawana elimu ya kutosha kuhusu usalama barabarani hali inayosababisha kuendelea kutokea kwa ajali zisizokuwa za lazima.

Alisema kuwa baadhi ya wapanda pikipiki wamekuwa wakikiuka taratibu kwa kutovaa kofia ngumu, kupakia abiria zaidi ya mmoja pamoja na kutokuwa na kofia ya abiria wake
Alinukuliwa akisema
“KUNA BAADHI WANAUTUHARIBIA UTARATIBU TULIOJIWEKEA WANAPAKIA ABIRIA ZAIDI YA MMOJA HASA NYAKATI ZA USIKU HALI INAYOWEZA KUSABABISHA AJALI.

Aidha amewashauri wapanda pikipiki kutovunja sheria za usalama barabarani kwani kufanya hivyo kunapelekea ajali zisizikuwa za lazima na kupoteza nguvu kazi ya taifa.
Pamoja na mambo mengine Bw Pashal alisema  kuwa wapanda pikipiki hao wanatarajiwa kufanya uchaguzi ili kupata viongozi wapya katika mkutano utakaofanyika katika ukumbi wa Community Centre mjini Ngara