Sunday, February 24, 2013

MURUSAGAMBA HATARINI KUKUMBWA NA NJAANGARA
Wakazi wa kijiji cha Murubanga kata ya Murusagamba wilayani Ngara huenda wakakumbwa na baa la njaa kutokana na kundi la tembo kushambulia zaidi ya ekari 60 za mahindi kijijini humo

Diwani wa kata ya Murusagamba Bw Soud Mkubila amesema kuwa tembo wanaokadiriwa kufikia 50 wamevamia eneo la Mulonzi yaliko mashamba mengi ya wakazi wa kijiji cha Murubanga

Amesema taarifa kuhusu uharibifu huo zimetolewa kwa halmashauri ya wilaya ya Ngara ili wataalamu wende kuwafukuza tembo hao waliovamia kijijini humo tangu juzi na kusababisha hofu kwa wanakijiji

Bw Mkubila amesema kuwa wataalam wa idara ya wanyamapori kutoka halmashauri ya wilaya ya Ngara wamekwenda kijijini humo leo kwa ajili ya kuwafukuza tembo hao na kufanya tathmini ya uharibifu uliojitokeza

No comments:

Post a Comment