Sunday, February 24, 2013

Wapanda pikipiki marufuku kupakia abiria zaidi ya mmoja
Mrisho Salum
Ngara-kagera
Katibu wa chama cha wapanda pikipiki wilayani Ngara Bw Castory Paschal amewataka wapanda pikipiki wilayani humo kujenga kawaida ya kutii sheria bila shuruti ili kuepuka mikwaruzano na vyombo vya sheria na kuepuka ajali zinazoweza kuepukika

Akizungumza na mjukuu wa tozo Bw Paschal amesema kuwa wapanda pikipiki wengi wilayani humo hawana elimu ya kutosha kuhusu usalama barabarani hali inayosababisha kuendelea kutokea kwa ajali zisizokuwa za lazima.

Alisema kuwa baadhi ya wapanda pikipiki wamekuwa wakikiuka taratibu kwa kutovaa kofia ngumu, kupakia abiria zaidi ya mmoja pamoja na kutokuwa na kofia ya abiria wake
Alinukuliwa akisema
“KUNA BAADHI WANAUTUHARIBIA UTARATIBU TULIOJIWEKEA WANAPAKIA ABIRIA ZAIDI YA MMOJA HASA NYAKATI ZA USIKU HALI INAYOWEZA KUSABABISHA AJALI.

Aidha amewashauri wapanda pikipiki kutovunja sheria za usalama barabarani kwani kufanya hivyo kunapelekea ajali zisizikuwa za lazima na kupoteza nguvu kazi ya taifa.
Pamoja na mambo mengine Bw Pashal alisema  kuwa wapanda pikipiki hao wanatarajiwa kufanya uchaguzi ili kupata viongozi wapya katika mkutano utakaofanyika katika ukumbi wa Community Centre mjini Ngara

No comments:

Post a Comment