Sunday, February 24, 2013

Wzazi wanaoshindwa kupeleka watoto shule kukamatwa-Ngara


Na. Mrisho Salum
NgaraSerikali wilayani ngara imeanza zoezi la kuwakamata wazazi ambao hawajawpeleka shule wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari kwa ajili ya chukuliwa hatua za kisheria.
 
Akizungumza na mwandishi wa habari hii ofisini kwake kaimu katibu tawala wa wilaya ya Ngara david mafipa amesema zoezi hilo litaanza katika kata za murukulazo,ntobeye na kumalizia kata ya kanazi.
 
Bw.Mafipa amesema kuwa asilimia 40 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu hawajaripoti katika shule walizopangiwa.
 
Alinukuliwa akisema
"TUTAWAKAMATA KAMA TULIVYO AHIDI NA TUWAPELEKA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA WAKAJIBU MASHTAKA,KAMA TULIVYOSEMA KWAMBA TUTAAKIKISHA HAKI ZA WATOTO WANAPATA IKIWEMO HAKI YA ELIMU NI WAJIBU WA MZAZI KUAKIKISHA MWANAE ANAKWENDA SHULE"
 
Aidha amesema zoezi hilo ni endelevu na litafanyika kwa wilaya nzima ili kuwabaini wazazi ambao wameshindwa kuwapeleka watoto wao shule kutokana na visingizio mbalimbali ili wafikishwe katika vyombo vya sheria
 
Kwa upande wao wananchi walikipongeza kitendo cha serikali wilayani ngara kuwachukulia hatua wazazi ambao hawajawpeleka shule watoto wao waliochaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari nakuiomba serikali ijizatiti kwa zoezi hilo kutokana na zoezi hilo kuwa gumu.
 
Mmoja ya wananchi Bw.Goerge Andrew alisema kuwa serikali inatakiwa kujizatiti vilivyo kwa ajili ya zoezi hilo
"Kiukweli serikali yetu imefanya jambo zuri kutokana na umuhimu wa elimu kwa watoto kwa sasa ila inatakiwa ijizatiti kutokana na wazazi wengine wasioelewa kuwaficha watoto ama kukimbia"

No comments:

Post a Comment