Na James jovin
KIBONDO
Paroko Christopher Ndizeye wa
parokia ya Kibondo mkoani Kigoma amewataka walimu kutambua kuwa ualimu ni wito
hivyo wanatakiwa kuifanya kazi hiyo kwa moyo na uzalendo ili kuinua kiwango cha
ufaulu kwa wanafunzi
Padre Ndizeye amesema hayo juzi
alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya tisa ya kidato cha sita katika shule
ya sekondari ya wasichana Bon Konsil wilayani Kibondo
Amesema iwapo walimu watafanya kazi
zao kwa moyo wa dhati na kuweka uzalendo mbele watasaidia wanafunzi kupenda
masomo hali itakayoinua kiwango cha taaluma nchini
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo
Sister Generoza Mpilirwe ametoa wito kwa serikali kutafuta kiini cha kushuka
kwa kiwango cha ufaulu kila mwaka na kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo
No comments:
Post a Comment