Tuesday, September 25, 2012

VAN PERSIE NA MASTAA WENGINE ENGLAND WALIVYOJIACHIA KWENYE CONCERT YA ALICIA KEYS



They may be rivals on the pitch but a number of Premier League stars joined forces on Monday night... for an Alicia Keys concert.
The American diva was performing in front of 1,000 fans at the 'MTV Crashes Manchester' show staged inside the city's cathedral.
Manchester United duo Robin van Persie and Alexander Buttner were joined by their partners for the gig.
Double act: Alexander Buttner (left) and Robin van Persie were all smiles at the concert
Double act: Alexander Buttner (left) and Robin van Persie were all smiles at the concert
Van Persie and Bouchra
Buttner and girlfriend
Party time: Van Persie and Buttner brought their partners along for the night out at Manchester Cathedral
Also there was Manchester City goalkeeper Joe Hart, who was accompanied by his girlfriend Kimberley Crew. Another City star - David Silva - joined them.
And Liverpool's 17-year-old sensation Raheem Sterling was another top-flight ace invited along to the bash.
He was there with his girlfriend Shana Ann Rose and tweeted: 'Alicia keys 1 word #PENG'.
Dutchmen Van Persie and Buttner have become good pals since they both arrived at Old Trafford in the summer.
Teenage kicks: Raheem Sterling wore an Amy Winehouse t-shirt alongside girlfriend Shana Ann Rose
Teenage kicks: Raheem Sterling wore an Amy Winehouse t-shirt alongside girlfriend Shana Ann Rose
Van Persie was joined by his wife Bouchra, while Buttner took his girlfriend along too.
The pair have both started well at United, with Van Persie their new spearhead up front and Buttner battling with Patrice Evra for the left-back slot.
Sterling is another player who has caught the eye this season. Despite Liverpool's woeful start to the season, the teenage winger has impressed with his dazzling performances under new boss Brendan Rodgers.
City boys: Joe Hart and David Silva (left) were among the crowd at the gig
City boys: Joe Hart and David Silva (left) were among the crowd at the gig
City gents: Pablo Zabaleta and Javi Garcia were also present at the concert
City gents: Pablo Zabaleta and Javi Garcia were also present at the concert
Star of the show: Alicia Keys on stage at Manchester Cathedral on Monday evening
Star of the show: Alicia Keys on stage at Manchester Cathedral on Monday evening


Read more: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2208284/Robin-van-Persie-Alex-Buttner-Joe-Hart-Raheem-Sterling-watch-Alicia-Keys-concert.html#ixzz27TpPfbJm
Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on Facebook

Mzungu aishitaki Yanga Fifa,kuna hatari ikashushwa daraja, Tff nayo yasema haitambui mabadiliko ya sekretariet


Papic kushoto akiwa na BIN ZUBEIRY enzi zake Yanga

Na Mahmoud Zubeiry
ALIYEKUWA kocha wa klabu ya soka ya Yanga ya Dar es Salaam, Kostadin Bozidar Papic amefungua mashitaka Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), dhidi ya klabu hiyo, akidai malimbikizo yake ya mishahara, dola za Kimarekani 12,300, zaidi ya Sh. Milioni 15 za Tanzania.   
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah Malabeja ameiambia BIN ZUBEIRY leo mchana kwamba, wamepokea barua kutoka Kitengo cha Sheria cha FIFA, kiwataka tuitaarifu Yanga kuhusu mashtaka yaliyowasilishwa na kocha wao huyo zamani, raia wa Serbia.
Angetile amesema Katika malalamiko yake, Papic anadai kuwa hajalipwa malimbikizo ya mshahara wake yanayofikia kiasi cha dola 12,300 za Kimarekani. Katika barua yake, kocha huyo anadai kuwa alikuwa akiwasiliana na maofisa na viongozi waYanga, lakini hakupata ushirikiano na hivyo kuamua kwenda FIFA.
Angetile alisema TFF ilifanya juhudi za kuwasiliana na Yanga kuhusu malalamiko hayo ili kujaribu kumzuia kocha huyo asishtaki FIFA, lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda.
“Na kama chombo kinachosimamia uendeshaji wa soka nchini, TFF imesikitishwa na habari hizo na inaiomba klabu ya Yanga kufanya kila jitihada kuhakikisha kuwa inawasilisha taarifa zote muhimu na nyaraka zinazohusiana na stahiki za kocha huyo ili kama ilishamalizana naye, sifa ya klabu ya Yanga isafishwe,”alisema Angetile.
Alisema tayari wamekwishaiandikia barua Yanga kuitaka itekeleze utashi huo mapema iwezekanavyo.
“Tukio hilo, si tu linachafua sifa ya klabu ya Yanga, bali soka ya Tanzania kwa ujumla kutokana na ukweli kwamba ikishadhihirika kuwa kuna tatizo la malipo ya makocha nchini, ni dhahiri kuwa itakuwa ni vigumu kwa klabu zetu na hata timu za taifa kupata makocha wazuri kutoka nje kwa kuwa watakuwa wamejengeka hofu ya kufanya kazi nchini,”alisema.
Hili ni tukio la pili kwa Yanga baada ya mchezaji wake mwingine, John Njoroge kuishtaki klabu hiyo FIFA na kushinda kesi yake iliyoamuliwa mwezi Januari na Kitengo cha Usuluhishi wa Migogoro cha FIFA (DRC).
Alisema ushindi wa Njoroge unamaanisha kuwa iwapo Yanga itashindwa kutekeleza kumlipa mchezaji huyo kasi cha Sh milioni 17, inaweza kujikuta katika adhabu ambayo itailazimisha TFF kuishusha daraja; kuinyang’anya pointi kwa kiwango kitakachotajwa na FIFA; kuipiga faini au adhabu zote kwenda kwa pamoja.
“Tunaiomba Yanga itekeleze hukumu hiyo kwa wakati uliotajwa kwenye barua ya FIFA ili kuepuka hatua hizo,  suala la Njoroge ni moja kati ya matukio mengi yanayohusu ukiukwaji wa taratibu za kuvunja mikataba yanayofanywa na klabu zetu.
Kuna malalamiko ya wachezaji wengi dhidi ya klabu zao za zamani kuhusu kutolipwa stahiki zao. Hivyo TFF inatoa wito kwa klabu kujiepusha na vitendo hivyo kwa kuwa vinawanyima haki wachezaji, lakini pia vinachafua sifa ya nchi iwapo wachezaji wanachukua hatua za kwenda kwenye vyombo vya juu,”alisema Wambura.
Aidha, Angetile amesema kwamba wamekuwa wakisoma kwenye vyombo vya habari kuhusu kutimuliwa kwa sekretarieti nzima ya Yanga kutokana na kuonekana kuwa ina udhaifu, lakini taarifa hizo hazijaifikia rasmi TFF.
Alisema kiutaratibu, Yanga inatakiwa iwsasilishe majina ya maofisa watakaofanya kazi na TFF kwa sasa na itakapoajiri sekretarieti ya kudumu, basi itume barua nyingine ya kuwatambulisha watendaji wake.
Alisema kama Yanga itakuwa imeitimua sekretarieti nzima, basi TFF inapokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kwani pamoja na kwamba si nia ya TFF kutetea watendaji wazembe, lakini klabu hazina budi kufuatilia kwa karibu utendaji wa sekretarieti zao ili isije ikafikia wakati sekretarieti nzima inaondolewa kwa makosa ambayo yangeweza kusahihishwa kama kungekuwa na ufuatiliaji wa karibu.
“TFF imekuwa ikitoa mafunzo kwa watendaji wa klabu ili waweze kufanya kazi zao vizuri na kwa mintaarafu ya mpira wa miguu na hivyo kuondolewa kwa timu nzima kama hiyo kunamaanisha kuwa ni upotevu wa rasilimali ambayo imetumika kuwapa elimu ya kutenda kazi zao vizuri. TFF ilishafanya kozi ya Event Management kwa ajili ya watendaji wa klabu; semina ya kuangalia upya maazimio ya Bagamoyo kwa watendaji na viongozi na pia kozi ya utawala hivyo haipendi juhudi hizi zipotee kirahisi,”alisema Angetile.
Chanzo Bin Zubeiry blogsspot

Kwa hili busara zinahitajika:Askofu Mokiwa na vurugu za waumini kanisa la Anglikana Sumbawanga.



Mmoja wa waumini wa kanisa la Anglikana la watakatifu wote la mjini Sumbawanga akiwa na jazba wakati wa vurugu zilizoibuka jana mara baada ya kutolewa uamuzi wa nyumba ya maaskofu wa kuridhia  askofu Mathayo Kasagara kuwa kiongozi wao ambapo vurugu kubwa zilizuka na kusababisha askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk Mokiwa kuondolewa akiwa chini ya ulizi wa polisi.


Na Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu.
Askofu  Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania  la  Dk. Valentino  Mkowa leo amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kunusurika kupata kipigo kutoka kwa waumini wake waliokuwa wenye hasira kali.
Vurugu kubwa ziliibuka mara  baada ya kusomwa kwa  tamko lililothibitisha kuwa nyumba ya maaskofu inamtambua  Askofu Canon Kasagara kuwa ni kiongozi wao halali wa kanisa la Anglikana la watakatifu wote Jimbo  la Ziwa Rukwa mjini Sumbawanga.
Katibu mkuu wa Anglikana Dk, Dickson Chilongani ndiye aliyesoma tamko hilo mara baada ya kumalizika kwa ibada iliyoongozwa na Askofu Mkuu Dk. Mokiwa.
Akisoma tamko hilo Katibu Mkuu alisema kuwa sehemu ya hoja za msingi kamati ya usimamizi wa kanisa hilo zilidai kuwa uchaguzi uliomweka madarakani Askofu Kasagara uligubikwa na rushwa,si za kweli na  nyumba ya maaskofu imeshindwa kuthibitisha hilo hivyo Kasagara ni askofu wao halali.

Askofu Mkuu wa Angikana Tanzania, la Dk. Valentino Mkowa aliyevuliwa kofia ya kiaskofu akiwa chini ya ulinzi wa polisi waliokuwa wamevalia kiraia wakimtoa nje ya Kanisa la Anglikana la watakatifu wote mjini Sumbawanga baada ya kuzuka kwa vuguru kubwa jana.

Kutokana na kauli hiyo waumini hao, walianza kupiga kelele ya kupinga maelezo hayo hali iliyosababisha mjumbe  wa Kamati ya kusimamia kanisa hilo Flugence Lusunzu aliposhika kinasa sauti na kueleza kuwa wanao ushahidi wa kutosha kuwa rushwa ilitumika kwenye kinyang’anyiro cha  uchaguzi huo uliofanyika zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Alidai kuwa uamuzi wa nyumba ya maaskofu haukuwapa fursa ya kusikiliza upande wa walalamikaji ili hali ushahidi upo wazi, kutokana kauli hiyo zilianza fujo zilisababisha askofu Mokiwa kutolewa lugha chafu, kuvuliwa kufia yake ya kiaskofu, huku wengine warusha viti ambavyo alivikwepa hado alipoondolewa akiwa chini ya polisi waliokuwa wamevalia kiraia.
Hali hiyo iliharibu amani iliyokuwa imetawala ndani ya Kanisa hilo ambapo uligeuka kuwa uwanja wa vita huku waumini wakisikika wakidai kuwa ni heri kanisa hilo lifungwe kuliko Askofu Kasagara kuliongoza.
Awali tangu nyakati za asubuhi, polisi waliovaa kiraia walitanda katika viunga vya kanisa hilo ambapo Askofu Mokiwa aliwasili na kulakiwa vizuri na waumini wake waliokuwa wakishangilia kwa nyimbo na mapambio.
Hata hivyo tayari waumini wa Kanisa hilo walionya kwamba askofu Kasagara asikanyage kwenye eneo hilo, kwani kufanya hivyo kunge hatarisha amani onyo ambalo upande wa askofu Kasagara walitii hivyo askofu huyo mwenye makazi yake wilayani Mpanda alibaki katika nyumba moja ya kulala wageni alikokuwa amefikia.
Mmoja wa waumini  Julius Michael alisema kwa kuwa waumini wa Jimbo la Rukwa hawamtaki askofu Kasagara hakuna sababu ya kuwalazimishwa lakini  nyumba ya maaskofu inapaswa kuangalia uwezekano wa kuligawa jimbo hilo.

Waumini wa Kanisa la Anglikana la watakatifu wote mjini Sumbawanga jana wakipiga kelele kupinga uamuzi wa nyumba ya maaskofu wa kuridhia  askofu Mathayo Kasagara kuwa kiongozi wao ambapo vurugu kubwa zilizuka na kusababisha askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk Mokiwa kuondolewa akiwa chini ya ulizi wa polisi. Picha zote na Mussa Mwangoka.

Tayari Serikali imegawa mkoa wa Rukwa na kuzaa ule wa Katavi sasa hakuna umuhimu wa kuwalazimisha waumini wampokee mtu wasiyemtaka nyumba ya maaskofu waanzishe jimbo katika mkoa huo mpya na aongoze Kasagara.
 Alisema iwapo watatumia nguvu kumuweka Askofu huyo Rukwa haitasaidia kitu kwani hawezi kuwaongoza watu wasiotaka kushirikiana nae.
Mgogoro katika Kanisa hilo umedumu kwa zaidi ya miaka miwili sasa ambapo siku za nyuma waumini hao  walimzuia  Askofu  Mkuu,  Dk  Valentino  Mkowa  kumsimika  Askofu  huyo  na  badala  yake  alisikimkwa  tarehe 16, Juni mwaka jana   Mjini  Mpanda.
Kutokana na kujitokeza kwa mgogoro huo, ilifunguliwa  kesi mahakamani ya Hakimu Mkazi Sumbawanga na waumini wa anglikana, Fulgence Rusunzu na Rojas Bendera  na wenzao 191 yenye  namba 11/2011 wakipinga kuchaguliwa kwa askofu Kasagala kuwa kiongozi wa Dayosisi hiyo.
Ambayo iliondolewa baada ya pande mbili zinazovutana kukubaliana kuwa baraza la maaskofu ndilo lenye dhamana ya kutatua mgogoro huo.

Chanzo;www.mwanawamakonda.blogspot.com