Na Mussa
Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania la Dk.
Valentino Mkowa leo amejikuta kwenye
wakati mgumu baada ya kunusurika kupata kipigo kutoka kwa waumini wake
waliokuwa wenye hasira kali.
Vurugu kubwa
ziliibuka mara baada ya kusomwa kwa tamko lililothibitisha kuwa nyumba ya
maaskofu inamtambua Askofu Canon
Kasagara kuwa ni kiongozi wao halali wa kanisa la Anglikana la watakatifu wote
Jimbo la Ziwa Rukwa mjini Sumbawanga.
Katibu mkuu
wa Anglikana Dk, Dickson Chilongani ndiye aliyesoma tamko hilo mara baada ya
kumalizika kwa ibada iliyoongozwa na Askofu Mkuu Dk. Mokiwa.
Akisoma
tamko hilo Katibu Mkuu alisema kuwa sehemu ya hoja za msingi kamati ya
usimamizi wa kanisa hilo zilidai kuwa uchaguzi uliomweka madarakani Askofu
Kasagara uligubikwa na rushwa,si za kweli na
nyumba ya maaskofu imeshindwa kuthibitisha hilo hivyo Kasagara ni askofu
wao halali.
Kutokana na
kauli hiyo waumini hao, walianza kupiga kelele ya kupinga maelezo hayo hali iliyosababisha
mjumbe wa Kamati ya kusimamia kanisa
hilo Flugence Lusunzu aliposhika kinasa sauti na kueleza kuwa wanao ushahidi wa
kutosha kuwa rushwa ilitumika kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi huo uliofanyika zaidi ya miaka
miwili iliyopita.
Alidai kuwa
uamuzi wa nyumba ya maaskofu haukuwapa fursa ya kusikiliza upande wa
walalamikaji ili hali ushahidi upo wazi, kutokana kauli hiyo zilianza fujo
zilisababisha askofu Mokiwa kutolewa lugha chafu, kuvuliwa kufia yake ya
kiaskofu, huku wengine warusha viti ambavyo alivikwepa hado alipoondolewa akiwa
chini ya polisi waliokuwa wamevalia kiraia.
Hali hiyo
iliharibu amani iliyokuwa imetawala ndani ya Kanisa hilo ambapo uligeuka kuwa
uwanja wa vita huku waumini wakisikika wakidai kuwa ni heri kanisa hilo lifungwe
kuliko Askofu Kasagara kuliongoza.
Awali tangu
nyakati za asubuhi, polisi waliovaa kiraia walitanda katika viunga vya kanisa
hilo ambapo Askofu Mokiwa aliwasili na kulakiwa vizuri na waumini wake
waliokuwa wakishangilia kwa nyimbo na mapambio.
Hata hivyo
tayari waumini wa Kanisa hilo walionya kwamba askofu Kasagara asikanyage kwenye
eneo hilo, kwani kufanya hivyo kunge hatarisha amani onyo ambalo upande wa
askofu Kasagara walitii hivyo askofu huyo mwenye makazi yake wilayani Mpanda
alibaki katika nyumba moja ya kulala wageni alikokuwa amefikia.
Mmoja wa
waumini Julius Michael alisema kwa kuwa
waumini wa Jimbo la Rukwa hawamtaki askofu Kasagara hakuna sababu ya
kuwalazimishwa lakini nyumba ya maaskofu
inapaswa kuangalia uwezekano wa kuligawa jimbo hilo.
Tayari
Serikali imegawa mkoa wa Rukwa na kuzaa ule wa Katavi sasa hakuna umuhimu wa
kuwalazimisha waumini wampokee mtu wasiyemtaka nyumba ya maaskofu waanzishe
jimbo katika mkoa huo mpya na aongoze Kasagara.
Alisema iwapo watatumia nguvu kumuweka Askofu
huyo Rukwa haitasaidia kitu kwani hawezi kuwaongoza watu wasiotaka kushirikiana
nae.
Mgogoro
katika Kanisa hilo umedumu kwa zaidi ya miaka miwili sasa ambapo siku za nyuma
waumini hao walimzuia Askofu
Mkuu, Dk Valentino
Mkowa kumsimika Askofu huyo
na badala yake
alisikimkwa tarehe 16, Juni mwaka
jana Mjini Mpanda.
Kutokana na
kujitokeza kwa mgogoro huo, ilifunguliwa
kesi mahakamani ya Hakimu Mkazi Sumbawanga na waumini wa anglikana,
Fulgence Rusunzu na Rojas Bendera na
wenzao 191 yenye namba 11/2011 wakipinga
kuchaguliwa kwa askofu Kasagala kuwa kiongozi wa Dayosisi hiyo.
Chanzo;www.mwanawamakonda.blogspot.com
No comments:
Post a Comment