Monday, July 30, 2012
Katibu wa chama cha soka wilaya ya Kakonko(FAKADI) hakiitambui Ligi ya jamii inayochezwa kata ya Kasanda
Katibu (FAKADI) Denisa Lazaro. |
Na:Issa
Ngumba Kakonko.
Katibu wa chama cha soka wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Denisa Lazaro,amesema hatambui ligi ya jamii iliyokuwa ikichezwa katika kata ya Kasanda na kusabisha kifo cha mchezaji Inocent Daniel aliyekuwa akichezea timu ya Kazilamihunda FC ,aliefia uwanjani wakati timu yake ilipokuwa ikichuana na timu ya Chilambo FC katika uwanja wa Kasanda.
Denisa amesema kuwa chama cha soka wilaya ya kakonko (FAKADI) hakitahusika na lolote kuhusina na tatizo hilo lililotokea katika mchezo huo,kwa kuwa ligi hiyo watu wa kasanda walishiriki chini ya uongozi wa soka kutoka wilaya ya kibondo.
Aidha amewataka kusimamisha ligi hiyo hadi pale watakapopata maelekezo kutoka uongozi wa chama cha soka wilaya ya kakonko (FAKADI) na si kuagizwa na uongozi wa soka wilaya ya kibondo(KDFA).
Katibu huyo wa FAKADI Denisa amesema kuwa tayari ofisi yake imepokea fomu za kugombea uongozi katika chama hicho na amewataka wadau kujitokeza kuchukua fomu hizo na kwamba fomu hizo zitalipiwa ada ya shilingi elfu 30 kwa ngazi ya uongozi na wajumbe shilingi elfu 20.
source www.mwanawamakonda.blogspot.com
Gazeti la Mwanahalisi lafungiwa
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
TAMKO LA SERIKALI
GAZETI LA MWANAHALISI LAFUNGIWA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelifungia kutochapishwa gazeti la MwanaHalisi kuanzia 30 Julai, 2012 kwa muda usiojulikana kutokana na mwenendo wake wa kuandika habari na makala za uchochezi, uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.
Katika matoleo yake hivi karibuni, gazeti la MwanaHalisi toleo Na. 302 la Jumatano Julai, 11 – 18, 2012 na toleo Na. 303 la Jumatano Julai 18 – 24, 2012 na toleo Na. 304 la Jumatano Julai 25 hadi 01 Agosti, 2012 na mengine yaliyotangulia yamekuwa yakichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.
Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi, ameitwa na kuonywa mara nyingi, lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii, pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.
Mhariri, mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha Katiba ya nchi yetu ambacho kinatoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutonukuu kifungu cha 30 cha Katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.
Uamuzi wa Serikali
Serikali imeamua kulifungia kutochapishwa kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi, kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, kifungu Na. (25) (i), adhabu hiyo itaanza tarehe 30 Julai, 2012 kwa mujibu wa Tangazo la Serikali (Government Notice) Na. 258 lililochapishwa katika Gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dar Es Salaam tarehe 27 Julai, 2012.
Serikali inawataka wamiliki, wahariri na wanahabari kuzingatia sheria, uzalendo, weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari katika kutekeleza wajibu wa kuhabarisha, kuelimisha na kutoa burudani kwa wananchi.
Kama ilivyoelezwa Bungeni wakati wa kuwasilisha Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni waandishi na watangazaji wa habari wanatakiwa kuhakikisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoandaa vinazingatia taaluma na kuweka mbele maslahi ya Taifa letu na uzalendo. Uhuru na haki ya vyombo vya habari uendane na wajibu.
Kuanzia sasa Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya habari ambavyo kwa maksudi vitatoa taarifa za uchochezi ambazo zitahatarisha hali ya amani na utulivu uliopo nchini mwetu.
Imetolewa na
OFISI YA MSAJILI WA MAGAZETI
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
Sunday, July 29, 2012
Tazama Yanga katika picha waki shangilia ubingwa wa Kombe la Kagame 2012
Kikosi cha Yanga kilicho tetea ubingwa wa kagame |
Saidi Bahanuzi mfungaji bora wa mashindano ya kombe la Kagame 2012 |
Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli na mashabiki wao |
Ubao wa matangazo wa uwanja wa Taifa ukionyesha matokeo ya mchezo |
Ally Mustapha akiudaka mpira |
Kocha wa Yanga TOM Santfiet kulia na kocha wa Azam Sittwart Hall kushoto wakizungumza baada ya mechi |
Wachezaji wa Yanga wakishangilia ubingwa wa Kagame 2012 |
Wachezaji wa Yanga wakishangilia Ubingwa wao baada ya kuilaza Azam magoli 2-0 |
Wachezaji wa Yanga wakiwaonyesha mashabiki ubingwa wa kagame |
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meki Sadik akimkabidhi nahodha wa Yanga Nadir Haroub ubingwa wa Kombe la Kagame |
Agrey Moris wa Azam na Hamis Kiiza wa Yanga wakigombania mpira |
wachezaji wakikimbiza kombe la kagame |
Saturday, July 28, 2012
Yanga ni Bingwa tena Kagame Cup yaipiga Azam 2-0
Klabu ya Soka ya Yanga leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wamefanikiwa kutetea vizuri Taji lao la Klabu Bingwa Afrika ya Mashariki na ya Kati walipoitandika Timu ngumu ya Azam FC bao 2-0 kwenye Fainali na kuendelea kubaki na kombe hilo la KAGAME baada ya kulitwaa Mwaka jana walipowafunga Mahasimu wao wakubwa Simba kwa bao 1-0.
Aidha Wafungaji wa Yanga leo ni Mastraika wao hatari sana, Hamisi Kiiza na Said Bahanuzi, ambao ndio walipachika bao za leo na kila mmoja kufikisha Bao 6 wakifungana na Teddy Etekiama wa Vita Club ya DRC kwa kuwa ndio Wafungaji Bora wa Mashindano haya.
Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Hamisi Kiiza katika Dakika ya 44 na Said Bahanuzi akapiga Bao la pili katika Dakika ya 90.
Mwenyekiti mpya wa Yanga, Yusuf Manji. |
Hakika hii ni chereko kubwa huko Jangwani kwa Mwenyekiti mpya wa Yanga, Yusuf Manji, na Kocha wao mpya Tom Saintfient kwani huu ulikuwa ni mtihani wao mkubwa wa kwanza tangu watwae nyadhifa zao hivi karibuni.
Kikosi cha Vita Club ya Congo DR. |
Katika Mechi ya awali ya kusaka Mshindi wa Tatu, Vita Club ya Congo DR iliifunga APR ya Rwanda bao 2-1.
WAGOMBEA ‘BUTI la DHAHABU.
-Teddy Etekiama [Vita Club]=Bao 6
-Said Bahanuzi [Yanga]=6
-Hamisi Kiiza [Yanga]=6
-John Bocco [Azam]=5
-Suleiman Ndikumana [APR]=3
-Preus [APR]=2
-Abdallah Juma [Simba]=2
Tangu 2002 rais wa Rwanda, Paul Kagame alipotangaza kudhamini zawadi ya washindi ya dola 60, 000, ambapo bingwa anapata dola 30,000, wakati mshindi wa pili Dola 20,000 huku yule wa tatu anapata dola 10,000, mpaka leo zawadi hizo hazijabadilika.
Source www.mwanawamakonda.blogspot.com
Tazama habari mbalimbali katika picha nzuri na za kuvutia
Hawa ni Ngombe wakipatikana Tanzania ,licha ya nyama yao kuwa tamu ila supa star kawa kuku’ |
Kucheza na mwinzio huwa raha sana hasa pale mnapokuwa mmepumzika kwa wanyama huwa ni jambo la furaha sana. |
Watanzania na Waafrika wengi kwa ujumla asili ya malezi ya mtoto ilikuwa inahusisha mtoto wa kunyonyeshwa na mama na pia kubebwa mgongoni hadi atakapofikia umri wa kuweza kutembea mwenyewe. |
Hapooo sasa patamu mdau’’97.9FM Ngara,Rwanda’’93.6 FM Kibondo na Burundi,94.2 FM Kasulu,Kigoma ujiji,Mashariki mwa DRC >>Sikilizeni RK live kwenye www.radiostationstz.com’ ‘’upate radha na utamu wa burudani,elimu na taarifa mbalimbali za kijamii,huku tukipanda mbegu za matumaini na JUKWAA LA MATUMAINI’ |
Duh! kaazi kwelikweli najiuliza mpaka sasa kesho kutwa ni miaka 50 ya UHURU lakini...MWANAMKE KWELI NI MWANAMKE..Picha inamuonesha mama akikabiliwa na majukumu mazito kama anavyoonekana katika picha hii.Ingawa mama huyu anakabiliwa na changamoto mbalimbali bado anaonekana mwenye furaha. |
Karibu Tanzania ,Katavi Hippo . |
Tupende wanyama wa nchi yetu kwa pamoja inawezekana . |
Hivi ni Vichali vya ndege watuamshao asubuhi kwa milio ya aina tofauti kuashiria kumepambazuka. |
Wednesday, July 25, 2012
Rais mpya wa Ghana kuimarisha utulivu.
Bw.John Dramani akiapishwa Mahakamani. |
Kiongozi
mpya wa Ghana John Dramani Mahama ameahidi kuimarisha hali ya utulivu kufuatia
kifo cha Rais John Atta Mills. Bw. Mahama mwenye umri wa miaka 53, aliapishwa
saa kadhaa baada ya Rais aliyekuwa na umri wa miaka 68 kufariki hospitalini
mjini Accra.
Upinzani
wa nchini humo umesifu kasi iliyotumiwa katika kufanya mabadiliko
yaliyomkabidhi Bw.Mahama mamlaka ya kuiongoza nchi ya Ghana na kusema kuwa ni
kuonyesha kuwa Ghana ina upevu Kidemokrasi.
Bw.
Atta Mills aliyeiongoza Ghana kuanzia mwaka 2009 alikua na saratani ya koo na
alikua na mipango ya kuwania muhula wa pili katika uchaguzi unaopangwa
kufanyika mwezi disemba.
Mwandishi
wa BBC mjini Accra, Sammy Darko anasema kuwa Rais aliyekabidhiwa wadhifa wa
Rais ataongoza kama Rais hadi wakati wa uchaguzi, ingawa haijafahamika kama
atasimama kama mgombea rasmi wa chama cha NDC(National Democratic Congress.)
Wakati
wa kuapishwa mbele ya kikao maalum cha Bunge kilichoitishwa kwa dharura,
Bw.Mahama aliahidi kuwahudumia raia wote wa Ghana. Punde baada ya kutangazwa
kuwa Rais, Bw.Mahama alitangaza maombolezi ya wiki nzima.
Kiongozi
wa upinzani wa chama cha New Patriotic Party Nana Akufo Addo amesema
ameahirisha kampeni za kugombea kiti cha Rais kwa heshima ya marehemu.
Mwenyekiti
wa NPP Jake Obetsebi-Lamptey amesifu jinsi mabadiliko yalivyofanywa kufuatia
kifo cha Rais.
Ingawa
kulikuepo na mjadala mkubwa kuhusu afya ya Bw.Atta Mills, suala hilo
halikugusiwa rasmi, wanaserma wandishi wa habari. Kiongozi huyo alikanusha
kuhusu maumivu na kusisitiza kua katika hali nzuri ya afya.
Kulingana
na msaidizi wa Rais, marehemu alilalamika kua na maumivu siku ya jumatatu jioni
na tangu hapo hali yake ikazidi kua mbaya.
Source:mwanawamakonda.blogspot.com
Thursday, July 19, 2012
Thursday, July 12, 2012
RATIBA YA CHELSEA YA MSIMU MZIMA
Chelsea Fixture
August
|
Barclays Premier League
|
02/02/2013
|
15:00
|
||
Barclays Premier League
|
09/02/2013
|
15:00
|
|||
Barclays Premier League
|
23/02/2013
|
15:00
|
March
2013
Show
last 5 matches and coverage
|
Competition
|
Fixture
|
Date
|
Kick-off
|
Status
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Barclays Premier League
|
02/03/2013
|
15:00
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
2012
September
2012
October
2012
November
2012
December
2012
January
2013
February
2013
|
Barclays Premier League
|
09/03/2013
|
15:00
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Barclays Premier League
|
16/03/2013
|
15:00
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Barclays Premier League
|
30/03/2013
|
15:00
|
April
2013
Show
last 5 matches and coverage
|
Competition
|
Fixture
|
Date
|
Kick-off
|
Status
|
Barclays Premier League
|
06/04/2013
|
15:00
|
|||
Barclays Premier League
|
13/04/2013
|
15:00
|
|||
Barclays Premier League
|
20/04/2013
|
15:00
|
|||
Barclays Premier League
|
27/04/2013
|
15:00
|
May
2013
Show
last 5 matches and coverage
|
Competition
|
Fixture
|
Date
|
Kick-off
|
Status
|
Barclays Premier League
|
04/05/2013
|
15:00
|
|||
Barclays Premier League
|
12/05/2013
|
15:00
|
|||
Barclays Premier League
|
Subscribe to:
Posts (Atom)