Saturday, July 28, 2012

Tazama habari mbalimbali katika picha nzuri na za kuvutia


Hawa ni Ngombe wakipatikana Tanzania ,licha ya nyama yao kuwa tamu ila supa star kawa kuku’


Kucheza na  mwinzio huwa raha sana hasa pale mnapokuwa mmepumzika kwa wanyama huwa ni jambo la furaha sana.

 


Anajulikana kama Tiger mnyama jamii ya chui lakini mabaka yake ni tofauti.

 


Moja ya vivutio vinavyoifanya Tanzania kuwa nchi ya kipekee duniani ni msimu wa kuhama wanyama jamii ya nyumbu toka mbuga za ngorongoro na serengeti ambao kila mwaka huvuka mto Mara kuingia nchini Kenya kwa ajili ya kupisha kiangazi. Hili ni moja ya tukio ambalo limeingizwa katika maajabu 10 ya asili duniani. Pichani ni baadhi ya nyumbu wakianza kuvuka.Mwanza: moja ya majiji masafi kabisa Tanzania huku kukiwa na adhabu kubwa kwa wote wanaoshindwa kuweka mazingira yao katika hali usafi. Ni kwa nini Mwanza au Moshi wameweza lakini majiji mengine kama Dar es Salaam bado yanaendelea kutokuwa na mazingira safi?


Watanzania na Waafrika wengi kwa ujumla asili ya malezi ya mtoto ilikuwa inahusisha mtoto wa kunyonyeshwa na mama na pia kubebwa mgongoni hadi atakapofikia umri wa kuweza kutembea mwenyewe.


Hapooo  sasa patamu mdau’’97.9FM Ngara,Rwanda’’93.6 FM Kibondo na Burundi,94.2 FM Kasulu,Kigoma ujiji,Mashariki mwa DRC >>Sikilizeni RK live kwenye www.radiostationstz.com’ ‘’upate radha na utamu wa burudani,elimu na taarifa mbalimbali za kijamii,huku tukipanda mbegu za matumaini na JUKWAA LA MATUMAINI’


Picha imepigwa nikiwa nimesimama "mtaa" uitwao NYAMIAGA wilayani Ngara mkoani Kagera, maana ipo juu kidogo na ni karibu na NYAMIAGA shule ya msingi'' kama sikosei.... …..HAPA NI HADITHI YA MVUVI NA SAMAKI WA DHAHABU bana !!!


Duh! kaazi kwelikweli najiuliza mpaka sasa kesho kutwa ni miaka 50 ya UHURU lakini...MWANAMKE KWELI NI MWANAMKE..

Picha inamuonesha mama akikabiliwa na majukumu mazito kama anavyoonekana katika picha hii.Ingawa mama huyu anakabiliwa na changamoto mbalimbali bado anaonekana mwenye furaha.


Karibu Tanzania ,Katavi Hippo  .Tupende wanyama wa nchi yetu kwa pamoja inawezekana .

Hivi ni Vichali vya ndege watuamshao asubuhi kwa milio ya aina tofauti kuashiria kumepambazuka.

source mwanawamakonda.blogspot.com

No comments:

Post a Comment