Thursday, July 12, 2012

Fainali urafiki cup:Simba,Azam kutoana jasho Taifa

Timu za soka za Tanzania bara Simba na Azam leo zitaoneshana kazi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kugombania ubingwa wa Urafiki cup (ujirani mwema).

Mchezo huo utakao chezwa majira ya saa moja jioni majira ya Afrika mashariki unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na timu hizo kuwa na mashabiki wengi jijini Dar es salaam.

Viingilio vimeshawekwa wazi ambapo VIP A itakuwa sh.30.000,VIP B 20,000, VIP C 15,000,  VITI VYA MANJANO10,000 na VITI VYA BLUU NA KIJANI itakuwa sh.5000.

Timu hizo zimefikia hatua ya fainali baada ya kuzitupa nje ya mashindano timu za Zanzibar all stars na Falcon zote za Nzanzibar

No comments:

Post a Comment