Monday, July 30, 2012

Katibu wa chama cha soka wilaya ya Kakonko(FAKADI) hakiitambui Ligi ya jamii inayochezwa kata ya Kasanda


Katibu  (FAKADI)  Denisa Lazaro.


Na:Issa Ngumba  Kakonko.

Katibu wa chama cha soka wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma  Denisa Lazaro,amesema hatambui ligi ya jamii iliyokuwa ikichezwa katika kata ya Kasanda na kusabisha kifo cha  mchezaji Inocent Daniel aliyekuwa akichezea timu ya Kazilamihunda FC ,aliefia uwanjani wakati timu yake ilipokuwa ikichuana na timu ya Chilambo FC  katika  uwanja wa Kasanda.

 

 

Denisa amesema  kuwa chama cha soka wilaya ya kakonko (FAKADI) hakitahusika na lolote kuhusina na tatizo  hilo lililotokea katika mchezo  huo,kwa  kuwa ligi   hiyo watu wa kasanda walishiriki chini ya uongozi wa soka kutoka  wilaya ya kibondo.

 

 

Aidha  amewataka kusimamisha ligi  hiyo hadi pale watakapopata maelekezo kutoka uongozi wa chama cha soka wilaya ya kakonko (FAKADI) na si kuagizwa na uongozi wa soka wilaya ya kibondo(KDFA).

 

 

Katibu huyo wa FAKADI  Denisa amesema kuwa tayari ofisi yake imepokea fomu za kugombea uongozi katika chama  hicho na amewataka wadau kujitokeza kuchukua fomu  hizo na kwamba  fomu hizo zitalipiwa ada ya shilingi elfu 30 kwa  ngazi ya uongozi na wajumbe shilingi elfu 20.

 

source www.mwanawamakonda.blogspot.com

No comments:

Post a Comment