Monday, July 9, 2012


 Hatarini kupata magonjwa ya maambukizi kwa kutupa taka ovyo

Afisa mtendaji Bw.Richard Talaswa wa kijiji cha sekei kinacho patikana ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Arumeru mkoani Arusha ameelezea chanzo cha kucheleweshwa kuzolewa taka za majumbani.

Akizungumzia swala hilo akiwa ofisini kwake leo asubuhi ameeleza kuwa ubovu wa gari la kuzolea taka ndio chanzo kikubwa cha taka kushindwa kuzolewa kwa wakati kijijini hapo.

Pia ameeleza kuwa mradi huo wa kuzoa taka za majumbani  unasimamiwa na kampuni binafsi na unashirikisha Kata tano ambazo ni Sokoni II,Moivo,Kiranyi,Kimnyaki na Ngaramtoni na walipata eneo la kutupia taka maeneo ya Kisongo  lakini walizuiwa kwa kile kilichoelezwa ni uchafuzi wa mazingira.

Bw. Talaswa aliendelea kueleza kuwa kitongoji cha Naurei ndicho mwathirika mkubwa wa tatizo hilo kutokana na kukaliwa na wakazi wengi  wakiwemo wafanya biashara.


Kwa upande wa wakazi wa kijiji hicho walipoulizwa kuhusiana na adha hiyo waliutupia uongozi kijiji lawama na kudai kuwa wamekuwa wakitozwa Sh.1000 kwa kila kaya kwa ajili ya kuzolewa taka lakini hawaoni kinachotendeka zaidi ya uchafuzi wa mazingira unaofanywa na wakazi kwa kuwa hawana eneo maalum la kutupa taka kijijini hapo.

Walipoulizwa kuhusiana na gari la kuzoa taka za majumbani walieleza kuwa lina bagua sehemu za kuzoa taka kwani wanazoa za barabarani na halipiti kila mara huku wakazi wa ndani ndaniwakiwa hawajui pa kuzipeleka taka hali inayopelekea kuwa hatarini kupata magonjwa ya kuambukiza.

Akijibu shutuma hizo afisa mtendaji bw.Talaswa amesema kuwa wanashulikia tatizo hilo na wameshazungumza na Bi na Bw. afya ili wapate gari la kuzolea taka  kutoka Halmashauri

Aidha amewataka wakazi kila mmoja kwa nafasi yake kuwa mlinzi wa mwenzake ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira

No comments:

Post a Comment