Saturday, July 28, 2012

Yanga ni Bingwa tena Kagame Cup yaipiga Azam 2-0


Yanga: Ally Mustapha 'Barthez', Stephano Mwasika, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro' (C), Kelvin Yondan, Athuman Idd 'Chuji', Rashid Gumbo, Haruna Niyonzima, Said Bahanunzi, Hamis Kiiza 'Diego', David Luhende - 29.

Akiba: Yaw Berko, Ladislaus Mbogo, Juma Seif 'Kijiko', Idrisa Rashid, Shamte Ally, Nizar Khalfan, Jeryson Tegete



Klabu ya Soka ya Yanga  leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wamefanikiwa kutetea vizuri  Taji lao la Klabu Bingwa Afrika ya Mashariki na ya Kati walipoitandika Timu ngumu ya Azam FC bao 2-0 kwenye Fainali na kuendelea kubaki na kombe hilo la KAGAME  baada ya kulitwaa Mwaka jana walipowafunga Mahasimu wao  wakubwa Simba kwa  bao 1-0.

Aidha Wafungaji  wa Yanga leo ni Mastraika wao hatari sana, Hamisi Kiiza na Said Bahanuzi, ambao ndio walipachika bao za leo na kila mmoja kufikisha Bao 6 wakifungana na Teddy Etekiama wa Vita Club ya DRC kwa kuwa ndio Wafungaji Bora wa Mashindano haya.

Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Hamisi Kiiza katika Dakika ya 44 na Said Bahanuzi akapiga Bao la pili katika Dakika ya 90.

Mwenyekiti mpya wa Yanga, Yusuf Manji.

 

Hakika hii ni chereko kubwa huko Jangwani kwa Mwenyekiti mpya wa Yanga, Yusuf Manji, na Kocha wao mpya Tom Saintfient kwani huu ulikuwa ni mtihani wao mkubwa wa kwanza tangu watwae nyadhifa zao hivi karibuni.


Kikosi cha Vita Club ya Congo DR.

 

Katika Mechi ya awali ya kusaka Mshindi wa Tatu, Vita Club ya Congo DR iliifunga APR ya Rwanda bao 2-1.

Azam FC : Deo Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Jabir Aziz, Tcheche, Salum Abubakar, John Bocco, Ibrahim Mwaipopo, Ramadhan Chombo

Akiba: Mwadini Ally, Samir Haji Nuhu, Joseph Owino, Odhiambo, Khamis Mcha, Mrisho Ngassa, Mwaikimba

 

WAGOMBEA ‘BUTI la DHAHABU.

-Teddy Etekiama [Vita Club]=Bao 6

-Said Bahanuzi [Yanga]=6

-Hamisi Kiiza [Yanga]=6

-John Bocco [Azam]=5

-Suleiman Ndikumana [APR]=3

-Preus [APR]=2

-Abdallah Juma [Simba]=2

 

Tangu 2002 rais wa Rwanda, Paul Kagame alipotangaza kudhamini zawadi ya washindi ya dola 60, 000, ambapo bingwa anapata dola 30,000, wakati mshindi wa pili  Dola 20,000 huku yule wa tatu anapata dola 10,000, mpaka leo zawadi hizo hazijabadilika.

Source www.mwanawamakonda.blogspot.com

No comments:

Post a Comment