Hali ya eneo mlipuko ulipotokea
Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea
Ulinzi umeimarishwa
Wanasualama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio
Magesa Mulongo akiteta na RCO wa Mkoa wa Arusha
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na wananchi
kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote
waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa.
Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika
eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa
tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa
Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
Eneo
lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia.
Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya waumini vikiwa
vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri wa
Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo.
Godbless Lema ambaye
ni mbunge wa Arusha na ametembelea eneo la kanisa lililolipuliwa na bomu na
kuwafariji wahanga wa tukio hilo. Akiongea kwa jazba na hasira na wananchi
waliopo eneo la tukio, Lema ameitumu serikali kwa mara nyingine na kudai kuwa
uzembe wa viongozi ndo chanzo cha matukio kama haya.
Hotuba fupi na nasaha zake zilikuwa zikisikika moja kwa moja kupitia Radio maria kabla ya kituo hicho kuamua kukatisha nasaha zake. Haijafahamika mara moja sababu za kukatishwa kwa hotuba yake.
Hotuba fupi na nasaha zake zilikuwa zikisikika moja kwa moja kupitia Radio maria kabla ya kituo hicho kuamua kukatisha nasaha zake. Haijafahamika mara moja sababu za kukatishwa kwa hotuba yake.
Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mulongo alifika eneo ambalo ndio kanisa la katoliki
lililolipuliwa na bomu lilipo na kuwafariji wahanga wa tukio la bomu.
RPC wa mkoa wa Arusha naye aliambatana na mkuu wa mkoa na alikuwa anatoa nasaha zake kwa wananchi. RPC ameeleza kuwa tukio hili ni la kigaidi. Katika maelezo yake, RPC amesema kuwa aliyehusika alijitokeza nyuma ya jengo kwa kujificha na kurusha bomu.
Amesema Polisi wanawasaka waliohusika na unyama huu na ameomba yeyote mwenye taarifa yoyote aisaidie polis.

Waliojeruhiwa mpaka
sasa ambao wapo katika hospitali ya mkoa
ya MOUNT MERU ni 42 .huku mmoja akiwa amefariki kutokana na mlipuko huo na
alitambulika kwa jina la REGINA LONING’O KURESOI mkazi wa ORASITY JIJINI
ARUSHA.
Kwa taarifa ambazo
mjukuu wa tozo imezipata ni kwamba Mpaka sasa mtu mmoja
anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi
No comments:
Post a Comment