Sunday, May 5, 2013

HILI HAPA NDILO KANISA LENYEWE LILILOPIGWA BOMU LEO NA HALI INAVYOENDELEA SASA ENEO LA TUKIO, ARUSHA


Polisi wakijaribu kuchunguza eneo bomu lilipolipukia leo asubuhi wakati wa misa ya kuzindua kigango hicho.iliyo katika kata ya olasiti na parokia ya burka

eneo lenye utepe ndipo kinachohisiwa kuwa bomu ndipo kilipotua na kulipuka katika Kanisa la Mt Joseph Olasiti Arusha ambapo Balozi wa Papa alikuwa akihudhuria ibada ya Kuzindua Parokia kanisani hapo.... 
eneo lenye utepe ndipo kinachohisiwa kuwa bomu ndipo kilipotua na kulipuka katika Kanisa la Mt Joseph Olasiti Arusha ambapo Balozi wa Papa alikuwa akihudhuria ibada ya Kuzindua Parokia kanisani hapo....
Umati wa  wananchi wa mkoa wa Arusha wakiwa njiani kuelekea kuangalia ndugu na jamaa zao waliokuwamo kwenye ibada hiyo inasadikika majeruhi zaidi ya thelathini na watano wapo hospitali huku kukiwa hakuna taarifa ya vifo.
 Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali huku wananch wakilitazama kwa mbali kutokana na tishio la kutokea kwa milipuko mingine ...Mtu mmoja  amekamatwa kuhusiana na tukio hilio wakati wengine wanasadikika kukimbia.
 Waumini  pamoja na baadhi ya wanacchi wakiwa katika hali ya taharuki  wasiamini nini kilichotokea  kutokana na mlipuko mkubwa  uliotokea asubuhi ya leo.
Polisi waki imarisha doria eneo la tukio   baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali kupatiwa matibabu zaidi ...Mpaka tunaondoka eneo la tukio Viongozi mbali mbali akiwemo mmbunge wa arusha walikuwemo eneo hilo

No comments:

Post a Comment