Friday, May 3, 2013

Mitihani kidato cha nne 2012 kusahihishwa upya!Matokeo yafutwa.

Kutoka Bungeni Dodoma tunaarifiwa kuwa baada ya matokeo ya kidato cha nne kuwa mabaya mwaka,hatimaye serikali imekubali mapendekezo ya awali ya tume ya uchanguzi ya matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana kufutwa na kusahihishwa upya kupitia mfumo wa usahihishaji wa mwaka 2011 haraka iwezekanavyo
Hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughuliki a sera na uratibu, Mhe. William Lukuvi, akitoa maamuzi ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu Pinda ya kuchunguza matokeo hayo.
 Ni kutokana na tume kubaini makosa NECTA.
Grading system iliyotumika mwaka 2012 ni mpya,na sio iliyotumika 2011.
YAFUATAYO YAMEAMULIWA NA BARAZA LA MAWAZIRI
1.Matokeo yote ya kidato cha nne 2011 yamefutwa.
2.Standardization ifanyike,ili yapangwe upya kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:-
-Juhudi za wanafunzi
-mfumo wa mwaka 2011 ndio utumike
-Ongezeko kubwa la shule nchini
-ongezeko kubwa la wanafunzi
3.Baraza ni marufuku kufanya mabadiliko yoyote ya mfumo wa grading bila kujadiliana na kushirikisha wadau wengine.
4.Mfumo wa grading wa 2012 ufutwe haraka na ule wa 2011 ndio utumike.
TUME BADO INAENDELEA NA KAZI NA RIPOTI ZAIDI ITATOLEWA.
No comments:

Post a Comment