Friday, January 18, 2013

AFCON 2013: KABUMBU LINAANZA JUMAMOSI!!


AFCON_2013-NA_KABUMBU_LIANZE 









>>AFCON 2013: DONDOO MUHIMU KWA KILA TIMU

AFCON 2013, Mashindano ya kusaka Taifa Bingwa Afrika, yanaanza Jumamosi Januari 19 huko Afrika Kusini na Nchi 16 zinawania Taji hilo.

 DONDOO MUHIMU ZA KILA NCHI-VIKOSI/MAMENEJA/REKODI:


KUNDI A
South Africa
JINA MAARUFU: Bafana Bafana
UBORA FIFA: 87
RANGI: Kijani na Dhahabu
REKODI BORA AFCON: Mabingwa 1996
MENEJA: Gordon Igesund Miaka 56– Ni Gwiji wa Soka Nchini Afrika Kusini baada ya kuwahi kuwa Meneja wa Klabu 7 Nchini humo. Alicheza Soka lake Nchini Austria na kuteuliwa Meneja Juni 2012.
NAHODHA: Bongani Khumalo – Baada ya kustaafu Mchezaji wa Everton Steven Pienaar, Bongani Khumalo ndie akapewa Unahodha. Ni Mchezaji wa Tottenham lakini yupo kwa Mkopo huko Ugiriki na Klabu ya PAOK.
NYOTA: Katlego Mphela – Ameichezea Bafana Bafana tangu 2005 na kufunga Bao 23 katika Mechi 47 appearances na Bao lake la kukumbukwa ni lile la Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara Mwaka 2009 alipopiga Frikiki tamu iliyoipeleka Mechi ya kutafuta Mshindi wa 3 na Spain kwenye Dakika 30 za Nyongeza.
KIKOSI:
MAKIPA: Itumeleng Khune (Kaizer Chiefs), Senzo Meyiwa (Orlando Pirates), Wayne Sandilands (Mamelodi Sundowns)
MABEKI: Siboniso Gaxa naTshepo Masilela (Chiefs), Thabo Matlaba and Siyabonga Sangweni (Pirates), Bongani Khumalo (PAOK), Anele Ngcongca (Genk), Thabo Nthethe (Bloemfontein Celtic)
VIUNGO: Reneilwe Letsholonyane na Siphiwe Tshabalala (Chiefs), Lerato Chabangu (Moroka Swallows), Kagiso Dikgacoi (Crystal Palace), Dean Furman (Oldham), Max Mahlangu (Helsingborg), Oupa Manyisa (Pirates), Thuso Phala (Platinum Stars), Thulani Serero (Ajax)
MASTRAIKA: Lehlohonolo Majoro na Bernard Parker (Chiefs), Katlego Mphela (Sundowns), Tokelo Rantie (Malmo)
Morocco
JINA MAARUFU: Lions of the Atlas
UBORA FIFA: 74
RANGI: Nyekundu
REKODI BORA AFCON: Mabingwa 1976
MENEJA: Rachid Taoussi – Ni Meneja mpya aliembadili Eric Gerets baada ya Morocco kuaibishwa na Mozambique katika Mechi ya Kwanza ya Mchujo ya AFCON 2013 walipochapwa 2-0 lakini yeye akaisaidia Morocco kushinda 4-0 katika Mechi ya Marudiano. Taoussi, Miaka 56, alijijengea sifa baada ya kuiwezesha Klabu ya Morocco Maghreb Fez kutwaa Mataji matatu ya CAF Kombe la Shirikisho, African Super Cup na Throne Cup.
NAHODHA: Nadir Lamyaghri –Ni Kipa wa muda mrefu wa Morocco.
NYOTA: Abdelaziz Barrada – Ni Kijana wa Miaka 23 Kiungo anaechezea La Liga na Klabu ya Getafe.
KIKOSI:
MAKIPA: Khalid Askiri (Raja Casablanca), Nadir Lamyaghri (Wydad Casablanca), Anas Zniti (Moghreb Fes)
MABEKI: Abderahim Chakir (FAR Rabat), Abdelatif Nousseir (Moghreb Fes), Issam El Adoua (Guimaraes), Mehdi Benatia (Udinese), Zakarya Bergdich (Lens), Ahmed Kantari (Brest), Abdelhamid El Kaoutari (Montpellier)
VIUNGO: Karim El Ahmadi (Aston Villa), Abdelaziz Barrada (Getafe), Chahir Belghazouani (Ajaccio), Younes Belhanda (Montpellier), Adil Hermach (Al Hilal), Kamal Chafni (Brest), Mehdi Namli (Moghreb Tetouan)
MASTRAIKA: Nordin Amrabat (Galatasaray), Youssef El Arabi (Granada), Oussama Assaidi (Liverpool), Abderrazak Hamdallah (Olympique Safi), Mounir El Hamdaoui (Fiorentina), Youssef Kadioui (FAR)
Angola
JINA MAARUFU: The Sable Antelopes
UBORA FIFA: 84
RANGI: Nyekundu na Nyeusi
REKODI BORA AFCON: Robo Fainali 2008 na 2010
MENEJA: Gustavo Ferrin – Ni Raia wa Uruguay.
NAHODHA: Manucho – Ni Mchezaji wa zamani wa Manchester United ambae sasa yupo Real Valladolid ya Spain.
NYOTA: Djalma Campos – Ni Fowadi anachezea FC Porto ingawa yuko kwa Mkopo kwa Kasimpasa ya Turkey.
KIKOSI:
MAKIPA: Lama (Petro Atletico), Landu (Recreativo Libolo), Neblu (Primeiro Agosto)
MABEKI: Amaro, Bastos and Dani Massunguna (Primeiro), Fabricio, Mingo Bille na Pirolito (InterClube), Marco Airosa (AEL Limassol), Lunguinha (Kabuscorp), Zuela (Apoel Nicosia)
VIUNGO: Dede and Gilberto (AEL Limassol), Manucho Dinis (Primeiro), Manuel (Aviacao), Miguel (Petro)
MASTRAIKA: Djalma (Kasimpasa), Geraldo (Parana), Guilherme Afonso (Vaduz), Manucho Goncalves (Real Valladolid), Mateus (Nacional), Yano (Progresso)
Cape Verde Islands
JINA MAARUFU: Blue Sharks
UBORA FIFA: 69
RANGI: Bluu, Nyeupe na Nyekundu
REKODI BORA AFCON: Mashindano yao ya kwanza
MENEJA: Lucio Antunes –
NAHODHA: Nando Maria Neves – Ni Sentahafu mwenye Miaka 34 anaechezea Klabu ya Daraja la Pili Chateauroux ya France ingawa ashacheza Soka Nchini Portugal, Switzerland, Tunisia, Qatar na Czech Republic.
NYOTA: Ryan Mendes – Ni Chipukizi wa Miaka 23 anaecheza huko France Klabuni Lille.
KIKOSI:
MAKIPA: Fock (Petro Atletico), Rilly (Mindelense), Vozinha (Progresso Sambizanga)
MABEKI: Carlitos (AEL Limassol), Fernando Varela (Vaslui), Gege (Maritimo), Guy Ramos (Waalwijk), Josimar (Dordrecht), Nando (Chateauroux), Nivaldo (Academica Coimbra), Pecks (Gil Vicente)
VIUNGO: Babanco and David Silva (Olhanense), Platini (Santa Clara), Roni (Fola Esch), Marco Soares (Omonia Nicosia), Stenio (Feirense), Toni Varela (Sparta Rotterdam)
MASTRAIKA: Djaniny (Olhanense), Heldon (Maritimo), Julio Tavares (Dijon), Ryan Mendes (Lille), Rambe (Belenenses)
KUNDI B
Ghana
JINA MAARUFU: Black Stars
UBORA FIFA: 30
RANGI: Nyeupe
REKODI BORA AFCON: Mabingwa 1963, 1965, 1978, 1982
MENEJA: James Kwesi Appiah – Baada ya kuwa na Mameneja wawili kutoka Serbia Ghana iliamua kumteua Mzalendo na huyo ni Mtumishi wa muda mrefu wa Ghana akiwa Nahodha wa Ghana kuanzia 1987 hadi 1992.
NAHODHA: Asamoah Gyan – Ana historia ya kupanda na kushuka kwa Nchi yake Ghana baada ya kuifungia Magoli muhimu likiwemo lile la ushindi dhidi ya USA katika Mechi ya Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia Mwaka 2010 kwenye muda wa Nyongeza lakini pia alikosa Penati dhidi ya Uruguay baada ya Luis Suarez kuudaka mpira katika Robo Fainali ya Kombe la Dunia Mwaka 2010.
Gyan sasa anachezea Klabu ya UAE, Falme za Nchi za Kiarabu, Al Ain.
KIKOSI:
MAKIPA: Daniel Adjei (Liberty Professionals), Fatau Dauda (Ashanti Gold), Adam Kwarasey (Stromsgodset)
MABEKI: Harrison Afful (Esperance), Jerry Akaminko (Eskisehirspor), Mohammed Awal (Maritzburg Utd), John Boye (Rennes), Kissi Boateng (Berekum Chelsea), Jonathan Mensah (Evian), John Paintsil (Hapoel Tel Aviv), Isaac Vorsah (Red Bull Salzburg)
VIUNGO: Albert Adomah (Bristol City), Anthony Annan (Osasuna), Kwadwo Asamoah (Juventus), Solomon Asante (Berekum), Christian Atsu (Porto), Emmanuel Agyemang Badu (Udinese), Derek Boateng (Dnipro Dnipropetrovsk), Mohammed Rabiu (Evian), Mubarak Wakaso (Espanyol)
MASTRAIKA: Emmanuel Clottey (Esperance), Asamoah Gyan (Al Ain), Richmond Boakye Yiadom (Sassuolo)
NYOTA: Kwadwo Asamoah – Ana Umri wa Miaka 24 na ni Mchezaji wa Mabingwa Italy, Juventus.
Congo DR
JINA MAARUFU: The Leopards
UBORA FIFA: 99
RANGI: Bluu na Nyekundu
REKODI BORA AFCON: Mabingwa 1968 na 1974
MENEJA: Claude Le Roy – Ni Mfaransa ingawa imeripotiwa amebwaga manyanga kuifundisha Congo, kitu ambacho amekikanusha.
NAHODHA: Tresor Mputu – Ni Mchezaji wa Miaka 27 ambae ni Mfungaji hatari.
KIKOSI:
MAKIPA: Robert Kidiaba (TP Mazembe), Bakala Landu (MK Etancheite), Parfait Mandanda (Charleroi)
MABEKI: Jean Kasusula (Mazembe), Larrys Mabiala (Karabukspor), Chancel Mbemba (Anderlecht), Cedric Mongongu (Evian), Issama Mpeko (Vita Club), Landry Mulemo (Kortrijk), Gabriel Zakuani (Peterborough)
VIUNGO: Dioko Kaluyituka (Al-Kharitiyath), Deo Kanda (Mazembe), Cedric Makiadi (Freiburg), Zola Matumona (Mons-Bergen), Tresor Mputu (Mazembe), Youssouf Mulumbu (West Bromwich Albion)
MASTRAIKA: Patou Kabangu (Mazembe), Yves Diba (Al-Raed), Domi Kumbela (Eintracht Brunswick), Tresor LuaLua Lomana (Karabukspor), Manzia Budje (Shark), Dieumerci Mbokani (Anderlecht), Luvumbu Nzinga (Rojolu)
Mali

JINA MAARUFU: The Eagles
UBORA FIFA: 25
RANGI: Njano, Nyekundu na Kijani
REKODI BORA AFCON: Washindi wa Pili 1972
MENEJA: Patrice Carteron
NAHODHA: Seydou Keita Aliichezea Barcelona kwa Miaka minne hadi Msimu uliopita na kutwaa Ubingwa wa La Liga mara 3 na Ubingwa wa Ulaya mara 2.
KIKOSI:
MAKIPA: Soumbeyla Diakite (Stade Malien), Mamadou Samassa (Guingamp), Aly Yirango (Djoliba)
MABEKI: Adama Coulibaly (Auxerre), Idrissa Coulibaly (Lekihwiya), Ousmane Coulibaly (Brest), Salif Coulibaly (Djoliba), Fousseyni Diawara (Ajaccio), Mahamadou Ndiaye (Vitoria Guimaraes), Adama Tamboura (Randers), Molla Wague (Caen)
VIUNGO: Samba Diakite (QPR), Cheick Fantamady Diarra (Rennes), Sigamary Diarra (Ajaccio), Seydou Keita (Aerbin Dalian), Mohamed Lamine Sissoko (Paris Saint Germain), Samba Sow (Lens), Kalilou Traore (Sochaux), Mahamane Traore (Nice), Sambou Yatabare (Bastia)
MASTRAIKA: Cheick Tidiane Diabate (Bordeaux), Modibo Maiga (West Ham), Mamadou Samassa (Chievo)
NYOTA: Modibo Maiga – Ni hatari kwa ufungaji lakini hatabiriki.
Niger
JINA MAARUFU: Gazelles
UBORA FIFA: 105
RANGI: Nyeupe
REKODI BORA AFCON: Raundi ya Kwanza 2012
MENEJA: Gernot Rohr – Ni Mjerumani mwenye Miaka 59.
NAHODHA: Moussa Maazou – Ni Mchezaji wa Miaka 28 anaechezea Klabu ya Tunisia, Etoile du Sahel.
KIKOSI:
MAKIPA: Moussa Alzouma (Garde Nationale), Daouda Kassaly (Chippa Utd), Saminou Rabo (Sahel)
MABEKI: Ismael Alassane, Kader Amadou na Mohamed Soumaila (Olympic), Mohamed Bachar and Luky James (AS Douane), Mohammed Chikoto (Marsa), Koffi Dankowa (Zarzis), Kourouma Fatogoma (Chabab)
VIUNGO: Issoufou Boubacar (clubless), Karim Konate (clubless), Issiakou Koudize (Garde Nationale), Idrissa Laouali (Mangasport), Amadou Mountari (Le Mans), Williams N’Gonou (LB 07), Souleymane Sakou (Olympic), Babacar Talatou (AmaZulu)
MASTRAIKA: Kamilou Daouda (Saoura), Issoufou Dante (Wydad Fes), Moussa Maazou (Etoile Sahel), Modibo Sidibé (clubless)
NYOTA: Daouda Kamilou – Ana Umri wa Miaka 25 na yupo Klabu ya Algeria JS Saoura.
KUNDI C
Nigeria
JINA MAARUFU: Super Eagles
UBORA FIFA: 52
RANGI: Kijani
REKODI BORA AFCON: Mabingwa 1980 na 1994
MENEJA: Stephen Keshi – Ni Nguli wa Soka la Nigeria na ameichezea Nchi yake mara 64 na aliichukua Nchi yake mara baada ya kushindwa kufuzu kuingia Fainali za AFCON 2012.
Amewahi pia kuwa Meneja wa Timu za Taifa za Mali na Togo.
NAHODHA: Joseph Yobo – Ni Sentahafu Veterani aliewahi kuichezea Everton na yupo Timu ya Taifa ya Nigeria kwa Miaka 12 na kucheza Mechi 89.
Yobo, Miaka 32, anaichezea Fenerbahce ya Turkey.
KIKOSI:
MAKIPA: Chigozie Agbim (Enugu Rangers), Austin Ejide (Hapoel Be’er Sheba), Vincent Enyeama (Maccabi Tel Aviv)
MABEKI: Efe Ambrose (Celtic), Elderson Echiejile (Braga), Azubuike Egwuekwe (Warri Wolves), Kenneth Omeruo (ADO Den Haag), Godfrey Oboabona (Sunshine Stars), Juwon Oshaniwa (Ashdod), Joseph Yobo (Fenerbahce)
VIUNGO: Reuben Gabriel (Kano Pillars), Nosa Igiebor (Real Betis), John Obi Mikel (Chelsea), Obiora Nwankwo (Calcio Padova), Fegor Ogude (Valerenga), Ogenyi Onazi (Lazio)
MASTRAIKA: Sunday Mba and Ejike Uzoenyi (Enugu), Emmanuel Emenike (Spartak Moscow), Brown Ideye (Dynamo Kyiv), Victor Moses (Chelsea), Ahmed Musa (CSKA Moscow), Ikechukwu Uche (Villarreal)
NYOTA: John Obi Mikel - Ana Miaka 25 na yupo Chelsea ambako ameshacheza Mechi 263.
Zambia
JINA MAARUFU: The Copper Bullets [Chipolopolo]
UBORA FIFA: 34
RANGI: Chungwa na Kijani
REKODI BORA AFCON: Mabingwa 2012
MENEJA: Herve Renard – Sasa ni Shujaa wa Zambia baada ya kuiongoza Nchi hiyo kutwaa Ubingwa wa Afrika Mwaka jana ambako walizifunga Timu kubwa za Senegal, Ghana na ivory Coast.
NAHODHA: Christopher Katongo – Ndio Mchezaji Bora wa BBC kwa Mwaka 2012.
KIKOSI:
MAKIPA: Daniel Munyau (Red Arrows), Kennedy Mweene (Free State Stars), Joshua Titima (Power Dynamos)
MABEKI: Hichani Himoonde, Francis Kasonde and Stoppila Sunzu (TP Mazembe), Emmanuel Mbola (Porto), Joseph Musonda (Golden Arrows), Davies Nkausu (SuperSport Utd)
VIUNGO: Isaac Chansa and Christopher Katongo (Henan Jianje), Rainford Kalaba and Nathan Sinkala (Mazembe), Noah Chivuta (Free State Stars), Felix Katongo (Petro Atletico), Chisamba Lungu (Ural Oblast), Mukuka Mulenga (Power Dynamos), William Njobvu (Hapoel Beer Sheba)
MASTRAIKA: James Chamanga (Liaojing Whowin), Emmanuel Mayuka (Southampton), Collins Mbesuma (Orlando Pirates), Jacob Mulenga (Utrecht), Jonas Sakuwaha (Al Merreikh)
NYOTA: Emmanuel Mayuka – Ndie alietwaa Buti ya Dhahabu AFCON 2012 na sasa yupo na Klabu ya England Southampton.
Ethiopia
JINA MAARUFU: Walya Antelopes or Black Lions
UBORA FIFA: 110
RANGI: Njano na Kijani
REKODI BORA AFCON: Mabngwa 1962
MENEJA: Sewnet Bishaw – Hii ni mara ya pili kwa yeye kuwa Meneja wa Ethiopia.
NAHODHA: Degu Debebe – Ni Sentahafu anaechezea Klabu ya Ethiopia Saint-George.
KIKOSI:
MAKIPA: Sisay Bancha (Dedebit), Zerihun Tadele (St George), Jemal Tassew (Coffee)
MABEKI: Abebaw Butako, Degu Debebe, Biadgelegn Elias na Alula Girma (St George), Berhanu Bogale, Aynalem Hailu and Seyoum Tesfaye (Dedebit)
VIUNGO: Behailu Assefa, Addis Hintsa na Minyahil Teshome (Dedebit), Shimeles Bekele na Yared Zinabu (St George), Dawit Estifanos (Coffee), Asrat Megersa (EEPCO), Yusuf Saleh (Syrianska)
MASTRAIKA: Adane Girma and Oumed Ukuri (St George), Fuad Ibrahim (Minnesota Stars), Getaneh Kebede (Dedebit), Saladin Said (Wadi Degla)
NYOTA: Adana Girma – Ni Mchezaji wa Saint-George na hatari kwa Mabao.
Burkina Faso
JINA MAARUFU: The Stallions
UBORA FIFA: 89
RANGI: Kijani
REKODI BORA AFCON: Nafasi ya Nne 1998
MENEJA: Paul Put – Ni Raia wa Belgium.
NAHODHA: Moumouni Dagano – Ni Mchezaji anaecheza Klabu ya Qatar Al-Sailiya na ndie mmoja wa Wafungaji Bora wa Mechi za Mchujo za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 kwa kufunga Bao 12.
KIKOSI:
MAKIPA: Daouda Diakite (Lierse), Germain Sanou (St Etienne), Abdoulaye Soulama (Asante Kotoko)
MABEKI: Mohamed Koffi (Petrojet), Bakary Kone (Lyon), Paul Koulibaly (Dynamo Bucharest), Mady Panandetiguiri (Antwerp), Henri Traore (Ashanti Gold)
VIUNGO: Charles Kabore (Marseille), Djakaridja Kone (Evian), Prejuce Nacoulma (Gornik Zabrze), Issouf Ouattara (Chernomorets Burgas), Jonathan Pitroipa (Rennes), Aly Rabo (Al Shorta), Florent Rouamba (Sheriff Tiraspol), Wilfried Sanou (Kyoto Sanga), Abdou Razack Traore (Lechia Gdansk), Alain Traore (Lorient)
MASTRAIKA: Wilfried Dah na Pierre Koulibaly (Al Dhaid Sharjah), Wilfried Balima (Sheriff Tiraspol), Aristide Bance (Augsburg), Moumouni Dagano (Al Siliya)
NYOTA: Alain Traore – Ni Kaka wa Mchezaji mdogo wa Chelsea, Bertrand, ambae anachezea Klabu ya Llorient.
KUNDI D
Ivory Coast
JINA MAARUFU: The Elephants
UBORA FIFA: 14
RANGI: All-orange
REKODI BORA AFCON: Mshindi 1992
MENEJA: Sabri Lamouchi – Ana Miaka 41, Lamouchi na ni chaguo la ajabu kuiongoza Ivory Coast baada ya kuwa Mchezaji wa Auxerre, Monaco, Parma, Inter Milan na Marseille pamoja na Timu ya Taifa ya France aliyoichezea mara 12.
NAHODHA: Didier Drogba – ndie Mchezaji anaetambulika sana kwa Ivory Coast na mwenye Rekodi safi ya Mabao kwa Nchi yake, Bao 59 kwa Mechi 90.
Baada ya kuibeba Chelsea kutwaa Ubingwa wa Ulaya Mwaka jana, Drogba sasa yuko China na Klabu ya Shanghai Shenhua.
KIKOSI:
MAKIPA: Boubacar Barry (Lokeren), Daniel Yeboah (Dijon), Ali Badra Sangare (Ivoire Academie)
MABEKI: Souleymane Bamba (Trazbonspor), Arthur Boka (Stuttgart), Emmanuel Eboue (Galatasaray), Igor Lolo (Kuban Krasnodar), Siaka Tiene (PSG), Kolo Toure (Manchester City), Ismael Traore (Brest/FRA)
VIUNGO: Max Gradel (Saint-Etienne), Didier Ya Konan (Hanover), Abdul Razak (Manchester City), Romaric Ndri Koffi (Real Zaragoza), Cheick Tiote (Newcastle), Yaya Toure (Manchester City), Didier Zokora (Trazbonspor)
MASTRAIKA: Wilfried Bony (Vitesse Arnhem), Didier Drogba (Shanghai Shenhua), Gervinho (Arsenal), Salomon Kalou (Lille), Arouna Kone (Wigan), Lacina Traore (Anzhi Makhachkala)
NYOTA: Yaya Toure – Ni Kiungo imara alieichezea Nchi yake mara 72.
Tunisia
JINA MAARUFU: The Eagles of Carthage
UBORA FIFA: 45
RANGI: Nyeupe
REKODI BORA AFCON: Mabingwa 2004
MENEJA: Sami Trabelsi – Ni Kocha mdogo mwenye Miaka 44 lakini ana uzoefu mkubwa baada ya kung’ara akiichezea Tunisia kati ya 1994 na 2001.
NAHODHA: Aymen Mathlouthi - Ni kipa mwenye Miaka 28 anaedakia Klabu ya Tunisia Etoile du Sahel na ameichezea Tunisia Mechi 38.
KIKOSI:
MAKIPA: Moez Ben Cherifia (Esperance), Aymen Mathlouthi (Etoile Sahel), Farouk Ben Mustapha (CA Bizertin)
MABEKI: Khalil Chammam and Walid Hichri (Esperance), Aymen Abdennour (Toulouse), Anis Boussaidi (Tavria Simferopol), Chamseddine Dhaouadi (Etoile), Fateh Gharbi (CS Sfaxien), Bilel Ifa (Club Africain)
VIUNGO: Youssef Msakni, Khaled Mouelhi na Mejdi Traoui (Esperance), Haten Baratli (Club Africain), Oussama Darragi (Sion), Chadi Hammami (Kuwait SC), Wissem Yahia (Mersin Idman Yurdu)
MASTRAIKA: Zouheir Dhaouadi (clubless), Hamdi Harbaoui (Lokeren), Issam Jomaa (Kuwait SC), Wahbi Khazri (Bastia), Saber Khlifa (Evian), Fakreddine Ben Youssef (Sfaxien)
NYOTA: Issam Jemaa – Ni Straika ambae aliwahi kuichezea Auxerre ya France lakini sasa yupo Nchini Kuwait ambae ameifungia Tunisia Bao 34 katika Mechi 70.
Algeria
JINA MAARUFU: Fennec Foxes, Desert Warriors
UBORA FIFA: 19
RANGI: Nyeupe
REKODI BORA AFCON: Mabingwa 1990
MENEJA: Vahid Halilhodzic – Ni Kocha kutoka Bosnia ambae ameanza kuifundisha Algeria tangu Juni 2011 na aliwahi kuipeleka Ivory Coast Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 lakini akatimuliwa Miezi minne tu kabla Mashindano hayo kuanza.
NAHODHA: Medhi Lacen – Ni Kiungo anaechezea Getafe ya Spain.
KIKOSI:
MAKIPA: Azzeddine Doukha (Harrach), Rais Mbolhi (Krylia Sovetov), Cedric Si Mohammed (Bejaia)
MABEKI: Essaïd Belkalem and Ali Rial (JS Kabylie), Carl Medjani and Mehdi Mostefa (Ajaccio), Liassine Cadamuro (Real Sociedad), Faouzi Ghoulam (Saint-Etienne), Rafik Halliche (Academica), Djamel Mesbah (AC Milan)
VIUNGO: Hameur Bouazza (Racing Santander), Ryad Boudebouz (Sochaux), Sofiane Feghouli (Valencia), Adlene Guedioura (Nottingham Forest), Foued Kadir (Marseille), Medhi Lacen (Getafe), Khaled Lemmouchia (Club Africain), Saad Tedjar (USMA)
MASTRAIKA: Mohamed Aoudia (Entente Setif), Yacine Bezzaz (CS Constantine), Islam Slimani (Belouizdad), Hilal Soudani (Guimares)
NYOTA: Sofiane Feghouli – Ni Chipukizi wa Miaka 23 anaechezea Valencia ya Spain na pia aliwahi kuchezea Timu za Taifa za Vijana za France kabla kurudi kwenye Nchi ya asili yake.
Togo
JINA MAARUFU: The Sparrow Hawks
UBORA FIFA: 71
RANGI: Njano
REKODI BORA AFCON: Raundi ya Kwanza 1972, 1984, 1998, 2000, 2002 na 2006
MENEJA: Didier Six – Ameshaichezea Timu ya Taifa ya France kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 1978 na 1982.
NAHODHA: Emmanuel Adebayor – Ndie nguzo ya Togo ambae ameifungia Bao 26 katika Mechi 54.
KIKOSI:
MAKIPA: Mawugbe Atsou (Maranatha), Baba Tchagouni (Dijon)
MABEKI: Serge Akakpo (Zilina), Sadat Ouro-Akoriko (Free State Stars), Vincent Bossou (Navibank), Djene Dakonam (Coton Sport), Donou Kokou (Maranatha), Abdoul-Gafar Mamah (Dacia), Senah Mango (Marseille), Dare Nibombe (Boussou Dur Borinage)
VIUNGO: Kodjo Ametepe (Maranatha), Komlan Amewou (Nimes), Sapol Mani (Batna), Moustapha Salifou (clubless), Prince Segbefia (Auxerre), Dove Wome (Free State Stars)
MASTRAIKA: Kalen Damessi (Lille), Thomas Dossevi (Chonburi), Serge Gakpe (Nantes), Fessou Placa (Agaza), Emmanuel Adebayor (Tottenham)
NYOTA: Bila shaka ni Adebayor!

No comments:

Post a Comment