Friday, January 18, 2013

ASAMOAH GYAN: SITOPIGA PENATI TENA - MAMA ALINIKATAZA

Gyan discovered you're not allowed to throw the ball between your legs (Getty) 
Michuano ya 29 ya AFCON  ikiwa imebakiza siku chache kabla ya kuanza, huku timu ya taifa ya Ghana ikiwa ni moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kunyakua ubingwa wa michuano hiyo kwa pamoja na timu za Zambia, Ivory Coast na Nigeria.

Ghana itakuwa ikiongozwa na nahodha Asamoah Gyan, lakini kwa hakika itakuwa ngumu kumuona mshambuliaji wa zamani wa Sunderland na Udinese akienda kupiga mpira wa penati ikiwa Black Stars watapata penati.

Sio kwa sababu nyingine yoyote bali binafsi - hayati mama yake mzazi alimwambia asipige. 

 KutokaBBC:
"Nimeamua kutokupiga penati kwenye mechi za timu ya taifa," Gyan alisema.
"[...] Nilisema miezi michache iliyopita kwamba sitopiga penati, kabla mama yangu hajafariki mwezi November 2011 aliniambia nisipige penati tena."
Kwanini hayati mama yake alimwambia maneno hayo ambayo yamelionyesha hakuwa anamuamini mwanae?? Gyan anajibu kwamba penati aliyokosa katika robo fainali ya kombe la dunia 2010 dhidi ya Uruguay, ambayo ingeifanya Black Stars kutinga nusu fainali ya WOZA 2010.

Pia katika michuano ya AFCON 2012, Gyan alikosa penati katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Zambia ambayo iliingia fainali na kuifunga Ivory Coast kisha kubeba ubingwa.

Ingawa mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 anaweza akalazimika kupiga penati ikiwa timu yake itakwenda katika hatua ya kupigiana penati ili kuamua mshindi.

No comments:

Post a Comment