Klabu
ya Liverpool iko mbioni kumsaini Chipukizi wa Barazil Philippe Coutinho
huku hatima ya Kinda wa Crystal Palace, Wilfried Zaha, kujulikana
Jumatatu na Meneja wa West Ham, Sam Allardyce, amefunguliwa mashitaka na
FA, Chama cha Soka England, kwa kukiuka Kanuni kufuatia kauli yake
dhidi ya Refa aliechezesha Mechi yao na Manchester United.
Liverpool na Mbrazil
Liverpool wako mbioni kusaini Mchezaji
wao wa Pili katika Dirisha hili la Uhamisho la Mwezi Januari baada ya
kutoa Ofa ya Pauni Milioni 8 kumchukua Kiungo wa Inter Milan Philippe
Coutinho.
Coutinho, Miaka 20, ambae ameichezea
Brazil mara moja na alichukuliwa na Inter Milan akiwa na Miaka 16 tu na
kubaki kwao Brazil kwa Mkopo hadi 2010 ambako ndio alitua Inter Milan na
kucheza Mechi 28 lakini Msimu uliopita alipelekwa Spain kuchezea
Espanyol kwa Mkopo.
Mchezaji mwingine alienunuliwa na
Liverpool hii Januari ni Straika kutoka Chelsea Daniel Sturridge
aliechukuliwa kwa Dau la Pauni Milioni 12.
Zaha
Crystal Palace > Arsenal au Man United
Habari za ndani zimedokeza kuwa Uhamisho
wa Wilfried Zaha wa Crystal Palace kwenda Manchester United au Arsenal
utajulikana mwanzoni mwa Wiki ijayo.
Ingawa Man United ndio inayopewa nafasi
kubwa kumchukua Kinda huyo, hasa baada ya Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo,
David Gill, kukiri kuwa wamekuwa wakimfuatilia, lakini pia Arsenal
wamekuwa wakimwinda.
Hata akiuzwa kwa sasa, Crystal Palace
imekuwa ikisisitiza kipengele cha kubaki na Mchezaji huyo hadi mwishoni
mwa Msimu ili awasaidie kuwapandisha Daraja.
Frazier
Sunderland > Cardiff City
Fraizer Campbell yupo mbioni kukamilisha Uhamisho wa £600,000 kutoka Sunderland kwenda Cardiff City.
Straika huyo wa zamani wa Manchester
United ambae ameichezea England mara moja amekuwa akiandamwa na tatizo
la Goti baada ya kuumia vibaya mara mbili katika Goti hilo hilo moja
ambalo limemfanya kiwango kushuka.
Meneja wa Sunderland, Martin O'Neill,
anategemewa kumnunua Danny Graham kutoka Swansea kwa Pauni Milioni 5 ili
kumbadili Frazier Campbell.
M'Vila
Rennes > QPR
Kiungo huyo wa Klabu ya Rennes ya France
ambae anathaminiwa kwa Pauni Milioni 7 anawindwa na Meneja wa QPR Harry
Redknapp lakini pia zipo Klabu nyingine zinazomwandama.
Akiongea kuhusu Yann M'Vila, Loïc Rémy amesema: "Ningependa aje QPR tuwe pamoja. Nishamwambia hapa ni pazuri."
Sam Allardyce ashitakiwa na FA
Meneja wa West Ham Sam Allardyce
amefunguliwa Mashitaka ya Utovu wa Nidhamu na FA, Chama cha Soka
England, kufuatia kauli yake mara baada ya Timu yake Jumatano iliyopita
kufungwa Bao 1-0 na Manchester United na kutupwa nje ya FA CUP.
Alardyce alidai uamuzi wa kuwanyima
Penati Uwanjani Old Trafford na kuwapa Man United Penati ni sababu ya
kucheza Uwanja wa Nyumbani.
Hata hivyo Penati waliyopewa Man United
ilipaishwa na Straika Wayne Rooney. Allardyce amepewa hadi Januari 23
kujibu Mashitaka hayo.
Penati ambayo West Ham wanaidai ni pale Fulbeki Rafael alipokontroli mpira na Paja na kisha kumgonga Mkononi.
Allardyce alikaririwa akisema: “Unaona
kila mara Old Trafford! Hamna tofauti kati ya kushika kwa Rafael na
Jordan Spence. Ila Spence anachezea West Ham, Timu ya ugenini na Rafael
ni Mchezaji wa nyumbani Old Trafford.”
Taarifa ya FA imesema: “Shitaka hili linahusiana na kuvunjwa kwa Kanuni ya FA E3.”
CHANZO SOKA IN BONGO
No comments:
Post a Comment