Friday, January 18, 2013

SIMBA WAPIGWA 3-1 NA TIMU YA JESHI LA OMAN


Mabingwa wa soka Tanzania, Simba walifungwa mabao 3-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya jeshi la Oman..
mechi ilichezwa Ijumaa jioni kwenye uwanja wa Qaboos complex jijini muscat.
Bao la simba lilifungwa katika kipindi cha pili na Haruna Moshi 'boban'.
Mwenyekiti wake Ismail Aden Rage alikuwa jukwaani pamoja na viongozi wengine wa Simba, Rahma Al Kharusi na Musleh Rawahi pamoja na kocha Talib Hilal wakiishuhudia simba ikizama mbele ya wanajeshi hao ambao kikosi chao kina wachezaji tisa wanaocheza timu ya taifa ya Oman.
Boban na wenzake wakishangilia goli
Washabiki wa Simba wakishangilia goli lilofungwa na Boban
Kaseja, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngassa, Sunzu wakiwa benchi huku wakizungumza na mfadhili wa safari yao Bi.Rahma na mwenyekiti wao Aden Rage.
Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage akiwa wenyeji wake huko Oman wakiangalia Simba ikisurubiwa na wanajeshi. (
PICHA NA SALEH ALLY WA CHAMPIONI/GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment