Friday, January 18, 2013

Vichekesho Mchanganyiko


Vichekesho na Bervone:
Jamaa mmoja alimzimikia demu Fulani akawa hajui aanze vipi, akaenda kwao huyo demu akamkuta anafua chupi…akamwambia anaomba maji ya kunywa, demu kuingia ndani tu jamaa akainua beseni na kunywa maji yaliyolowekwa zile chupi…demu akaruka “nini sasa?” Jamaa akamjibu nyama hatuli, supu pia tusinywe?
mlevi mmoja alianguka nje ya geti la TBL msamaria mmoja akashauri wampe maji, mara mlevi akaropoka we mjinga nini? Ningetaka maji si ningeangukia geti la IDARA YA MAJI?
Mke anamwambia Mume wake “Niambie kitu kitakachonifurahisha na kuniudhi wakati huo huo! Mumewe akamwambia “Wewe ni mt**u  na unajua kunibembeleza kuliko marafiki zako wote.
........................................................................................................................

Mtaalam wa computer
akitongoza
dem.......!! penzi langu lina GB
kubwa sana kwako,mpenzi
nataka ni install moyo
wangu kwenye CPU ya nafasi
yako.Naomba uni-double
click
kwenye maisha yako niwe
software moyoni
mwako,ur life will not be at risk...condom
itakua
ni antivirus tosha....twende
angaza tukaji-scan
laazizi....!!!!
.................................................................................................
Bibi Mmoja Hivi Na Kofia Yake Iliyoleta Balaa!!
Bibi mmoja alikuwa
kwenye meli amevaa kofia
ghafla upepo ukavuma bibi
akashika kofia kwa
mikono miwili gauni nalo
likapeperushwa na upepo mtu mmoja
akamuuliza
unashika kofia wakati chini
kuwazi? Bibi akajibu uchi
ninao miaka 85 lakini kofia
nimenunua jana tu.
.............................................................................................................................................
Vitendawili na Methal>>Daah Wahindi Nomaa Wanaharibu Kiswahili Yetu!!
Jamani wahindi
wanatuharibia lugha.
Washatoka tution ya
kiswahili Mtu anajibu
vitendawili,methali na
mafumbo jinsi hiii .................. (1) Mfa maji?
… tampa life jacket. (2) Mwenda pole?…
tachelewa fika. (3) Usipoziba ufa ?…mizi
taona mpaka dani. (4) Usilolijua?…uliza
google.com. (5) Mbio za utelezini?…
chafua guo yako. (6) Ukipenda boga?…
ngoja
mezi ya ramzani tapata. (7) Ukiona
vinaelea?…iko
nyepesi hiyo. (8) Maji yakimwagika?…
mambie dada ta-deki. (9) Chelewa
chelewa?…
takosa guo ya sukukuu….. (10) Kila
ndege .....? Hutua
Airport (11) Bandu bandu ....?
Menzie Makame.... (12) Mtaka cha
Mvunguni ....? Binua tanda
ote 13) Simba mwenda
kimya .....? Iko gonjwa
kama sio gonjwa iko
fungwa na Yanga (14) Aisifuye mvua ....?
Mkulima (15) Barabara ndefu ....?
Ongeza mwendo, tachelewa
fika (16) Mla nawe hafi nawe
ila .....? Takimbia (17) Asie sikia la
mkuu ....?
Tapeka jela (18) Hasira za mkizi ....?
Tatafuna veve (19) Ujanja mwingi....?
Hapana mpa kazi taibia
yeye (20) Akumurikae
mchana ....? Iko pofu (21) Mficha
maradhi ....?
Taenda Loliondo (22) Mkataa wingi ....?
Taenda Chadema (23) Bendera ....? Kama
sio
ya CCM, ya CUF (24) Baniani mbaya ....?
Sio
kweli, naonea tu yeye 25) Akili nyingi ….?
Tapasi
mtihani.
.................................................................................................
Mwl wa kiswahili
akimtokea chick;
''Penzi langu kwako ni
KONGWE kama fasihi cmuliz''
''kwan nakupenda kama
NGOSWE alIvyompenda MAZOEA''
wala cna madem weng
kama JOTI nawe ucwe na
tabia kama za FURAHA wa
orodha cntakutenga kama
TAKADINI cos cna dhiki km MAMA NTILIE
bali ntakupa
maneno matam km
MALENGA WAPYA na
ntakuliwaza kwa mashahiri
kama ya WASAKA TONGE
napenda 2we pa1 kama KIIMA na KIARIFU
ktk
sentenc ili penz le2 lidumu
kama FASIHI ANDISHI vp
uko tayar 2fanye
UAMBISHAJI Walimu wengine bwana!

.....................................................................................................

JAMAA Kanunua mashine ya kukamulia ng'ombe MAZIWA, kabla ya kuitumia kwa ng'ommbe akaijaribu mwenyewe kwa kuivaa kwenye NANII yake, akasikia rahaaaa .....kuliko akinanii kwa mke wake

ILA alipomaliza akashangaa mashine haitoki, ikabidi apige simu dukani aliponunua..

JAMAA:aisee si nlijaribia kwenye naniliu yangu sasa nisha maliza haitoki

MUUZAJI: ebooo,hiyo ni automatiki mpaka ikamue LITA 1 NDIO ITOKE.
......................................................................................................
Prakata tumba tumba
KIBAKA alimpiga roba bubu, bubu akawa anajitetea kwa kupiga kelele:
Bubu: Abaabaabaabaa.
Kibaka, ili asijulikane kama anamkaba alimalizia naye kwa sauti ili ionekane wanaimba wimbo.
Kibaka: Prakata tumba…tumba.
......................................................................................................
Jisaidie tena umalizie fedha yako
ASKARI wa jiji alimkamata raia akijisadia haja ndogo hadharani tena mahali palipoandikwa USIKOJOE HAPA, FAINI SH. 5000. Raia huyo bila ubishi akatoa noti ya shilingi elfu 10 na kusubiri chenji. Askari alizunguka na kukosa chenji, akamrudia raia huyo na kumwambia:
Askari: Hebu kojoa mara ya pili umalizie fedha yako, nimekosa chenji.
...................................................................................................... 
Mume wangu anakuja sasa hiviMtu na mkewe walikuwa wamelala, katikati ya usiku mke akaanza kuweweseka na kusema:
“We! Amka, tena uondoke haraka sana mume wangu anakuja sasa hivi.”
Mara mume wake alikurupuka, akanyakua nguo zake na kurukia dirishani mpaka nje. Akiwa huko nje akakumbuka kuwa alikuwa amelala nyumbani kwake, akasema:
“Aah! Kumbe leo nimelala kwangu, sasa nilikuwa nakimbia nini?” akarudi.
Je, hapo nani msaliti kwa mwenzake?
....................................................................................................... 
Mtoto mwenyewe njiti bado unambemenda!
Siku moja Mzee wa Chabo alipumzika nyumbani, alilala muda mrefu alipoamka, asilimia kubwa ya wapangaji walikuwa wamekwenda kazini na kubaki wake zao.
Alichukua maji na kwenda chooni, akiwa anataka kutoka alishangaa kumuona mke wa jirani yake ambaye mumewe ni dereva wa magari makubwa aliyekuwa safarini nje ya nchi, akiingia kwenye chumba cha mpangaji mwingine asiye na mke huku amembeba mtoto wake mdogo ambaye alimzaa njiti.
Uingiaji wake ulimtia shaka na kutaka kujua anafuata nini kule, alitoka msalani na kusubiri kidogo, akazunguka nyuma ya nyumba na kupiga chabo dirishani. Alikuta mchezo umeanza, mtoto akiwa amelazwa kwenye kochi.
Kutoka nje ya ndoa haikumuuma Mzee wa Chabo bali yule mwanamke kumbembenda mwanaye aliyemzaa njiti.
Bila kutarajia, midomo yake ilisema kwa sauti:
“Mtoto mwenyewe njiti bado unambemenda!”
Utanisaidiaje daktari?
........................................................................................................
MVUTA bangi alikwenda kwa daktari na kumwambia.
“Mara nyingi huwa nazungumza na watu, lakini cha kushangaza watu hao huwa siwaoni, utanisaidiaje daktari?”
Daktari: “Ni wakati gani huwa inakujia hali kama hiyo?”
Mvuta bangi: “Mara nyingi pale ninapoongea nao kwa simu.”
Daktari nusura amwitie askari ili wamtoe balu.
 
source bongo hot zone
 

No comments:

Post a Comment