Lionel
Andres Messi anazidi kuishangaza dunia kwa uwezo wake mkubwa karika
soka. Lionel Messi aliezaliwa miaka 25 huko Rosario , Argentina. Messi
ni mtoto wa Mzee Jorge Horacio Messi ambae alikuwa mfanyakazi wa kiwanda
cha Chuma na mama yake Celia Maria Cuccitti. Kwa upande wa Baba yake
Messi anaasili ya Italy tokea mji mmoja unaitwa Ancoma, ambako ilikuwa
ni asili ya babu yake aitwae Angelo Messi aliehamia Argentina mwaka
1883. Messi ana kaka wawili na dada mmoja.
Katika
umri wa miaka mitano Leo Messi alianza kucheza soka katika club ya
Grandoli. Hii ilikuwa klabu ya mtaani kwao iliyokuwa inasimamiwa na Baba
ake. Mwaka 1995 Messi alihamia katika klabu ya Newell's Old Boys
iliyopo katika mji wake wa Rosario.
Messi akiwa na miaka 11 |
Raxach
alikubali kumpa Messi mkataba na Barcelona, akiwa hana karatasi yoyote
mkononi alimwandikia mkataba wa kwanza Messi katika Leso.
Hatimaye
Barcelona walikubali gharama za matibabu ya Messi kwa masharti kuwa
ahamie Hispania. Bila kipingamizi Messi na Baba yake wote wakahamia
Hispania na Lionel akaanza kuitumikia klabu ya Barcelona akiwa katika
katika shule ya vipaji ya klabu hiyo iliyo maarufu sana kama La Masia.
Messi na Macarena |
Inasemekana
Messi amewahi kuwa na uhusiano na mwanadada Macarena ambae naye
anatokea katika mji wa Rosario. Messi alitambulishwa kwa Rosario na
baba yake Rosario kipindi aliporudi kuuguza majeraha yake kabla ya
kuanza kwa Kombe la Dunia 2006. Messi pia alishawahi kuwa na uhusiano na
mwanamitindo wa Argentina mwanadada Luciana Salazaar.
Januari
2009 katika mahojiano ya kipindi "Hat-Trick Barca'" cha Canal 33 Messi
alisema anauhusiano na mwanamke mmoja hivi (hakumtaja jina) na anafuraha
kuwa nae swali hilo lilikuja baada ya Messi kuonekana katika sehemu
mbalimbali na mwanadada Antonella Roccuzzo. Juni mwaka 2012 Messi
akicheza mechi dhidi ya Ecuador alifanikiwa kufunga goli, alishangilia
Goli hilo kwakuweka mpira ndani ya jezi yake kuashiria kuwa mpenzi wake
ni mjamzito. Siku kadhaa baadae ikaripotiwa na vyombo vya habari kuwa
mpenzi wake ana ujauzito wa wiki 12 (miezi 3). Mnamo Tarehe 2 Novemba
mwaka 2012 mtoto wa kwanza wa Messi alizaliwa na kupewa jina la Thiago.
Messi akishangilia bao dhidi ya Ecuador |
Messi
ana ndugu wawili ambao waacheza mpira. Maxi anaichezea klabu ya Club
Olimpia nchini Paraguay na Emmanuel Biancucchi. Pamoja na kuishi Spain
kwa muda mrefu ila Messi hajaacha kupakumbuka Rosario. KIla mara
hutembelea mji huu na pia ana mawasiliano na marafiki na ndugu kadhaa
wanaoishi katika mji huo. Inasemekana wakati mmoja Argentina ilipokuwa
ikifanya mazoezi mjini Buenos Aires. Messi aliendesha mwendo wa masaa
matatu baada ya mazoezi kwenda Rosario kula chakula cha jioni na kulala
na kesho yake kugeuza mapema kabla ya mazoezi. Messi bado anamiliki
nyumba yao ya zamani ambako alikuwa anaishi na familia yake japokuwa
hakuna mwanafamilia anayeishi hapo siku hizi.
Mwaka 2007, Messi ameanzisha Charity Foundation kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wenye uhitaji.
Messi
alitangazwa kuwa balozi wakujitolea wa UNICEF katika maswala ya
kupigania haki za watoto. Barcelona nao wako nyuma wanamsaidia messi
katika hili kwakuwa Barcelona na Messi wana uhusiano mzuri.
Messi
alianza kuichezea timu ya wakubwa ya Barcelona tarehe 16 Novemba mwaka
2003 akiwa na umri wa miaka 16 na siku 145 katika mchezo wa kirafiki
kati ya Barcelona na F.C Porto ya Ureno.
Miezi
michache baadae Frank Rijkaard kocha wa barcelona kipindi hicho
alimpatia Messi nafasi ya kucheza ligi ya Spain dhidi ya RCD Espanyol
akiwa na Umri wa miaka 17 na siku 114 hivo kumfanya Messi kuwa mchezaji
wa tatu mwenye umri mdogo kuichezea Barcelona na mdogo kabisa kuichezea
Barcelona katika ligi. Rekodi ambayo baadae ilikuja kuvunjwa na Bojan
Krikic. Goli la kwanza la Messi katika timu ya wakubwa alilifunga dhidi
ya Albacete Balompie mwezi Mei mwaka 2005. September mwaka huohuo Messi
alipata urai wa Spain.
Baada
ya hapo amekuwa akicheza kwa mafanikio makubwa. Messi katika kipindi
hichi chote toka alipoanza kuichezea Barcelona amepata mafanikio mengi.
Mafanikio Binafsi kama mchezaji na Mafanikio ya timu pia.
Messi
ameweza kuvunja rekodi nyingi ambazo ziliwekwa na magwiji wa soka wa
zamani. Tukianzia katika klabu yake Messi ameweka rekodi ya kuwa
mchezaji anaeongoza kwa kufunga mabao mengi katika historia ya klabu
hiyo akiwa na magoli 283 na pia ni mchezaji alieifungia Barcelona mabao
mengi katika ligi ya Hispania uku akiwa na mabao 192. Messi anashikilia
rekodi ya klabu yakufunga Mabao mengi kwenye msimu mmoja akiwa amefunga
magoli 73 katika msimu wa 2011-2012. Messi anashikilia rekodi ya
Barcelona ya mchezaji aliefunga magoli mengi katika mashindano ya ulaya
akiwa na magoli 57 na 56 katika ligi ya mabingwa ulaya. Messi anaongoza
listi ya mchezaji aliefunga magoli mengi katika Spanish Super Cup akiwa
na magoli 10.
Messi
ana rekodi ya kuwa mchezaji alieifunga magoli mengi kwa msimu mmoja
katika michuano ya mabingwa ulaya akiwa na magoli 14, Messi huyuhuyu ana
rekodi ya kufunga magoli mengi katika mchezo mmoja wa ligi ya mabingwa
ulaya akiwa amefunga 5 katika mechi dhidi ya Bayern Leverkusen msimu wa
2011-2012. Messi ana rekodi pia yakufunga hat-tricks nyingi ndani ya
msimu mmoja akiwa amefunga hat-trick mara 8 msimu wa 2011-2012. Na bila
kusahau Messi anashikilia rekodi ya Barcelona ya kufunga magoli mengi
katika ile michuano ya klabu bingwa ya dunia akiwa na magoli 4.
Kwa
ujumla Messi anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliefunga magoli mengi
katika msimu mmoja wa ligi ya hispania akiwa amefunga magoli 50 katika
msimu mmoja. anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi katika msimu
mmoja wa ligi ya mabingwa huko akiwa a magoli 14 na pia anashikilia
rekodi ya kuwa mchezaji aliefunga magoli mengi ndani ya msimu mmoja
akiwa na magoli 73 katika mashindano yote. Messi hajaishia hapo, Jana
tarehe 09-Dec-2012 Messi amevinja rekodi ya mkongwe Gerd Muller ya mabao
85 katika mwaka mmoja ambayo ilidumu kwa miaka 40. Messi amefunga goli
la 85 na 86 jana akiisaidia Barcelona kushinda mchezo wake dhidi Real
Betis. Messi ameweka rekodi hiyo mpya uku akiwa na michezo mitatu mpaka
mwisho wa mwaka.
Messi
bado ana rekodi zake binafsi. Messi ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa
mwaka kwa miaka 3 mfululizo (209,2010,2011) na mwaka huu yuko katika
ile tatu bora. Messi anashikilia tuzo ya mfungaji bora wa bara la Ulaya
ya mwaka 2010 na mwaka 2012. Mshambuliaji bora wa ligi ya Hispania mwaka
2009,2010,2011,2012. Mchezaji bora wa ligi ya hispania mwaka
209,2010,2011,2012. Mfungaji bora ligi ya Mabingwa ulaya mwaka
2009,2010,2011 na 2012. Man of the match fainali ya ligi ya mabingwa
mwaka 2011.
SOURCE:http://valetyno.blogspot.ca/
No comments:
Post a Comment