Na
Mrisho Salum-NGARA
Chama
cha NCCR-Mageuzi mkoani Kagera kimemsimamisha mwenyekiti wa chama hicho
wilayani Ngara Bw Kennedy Stanford Festo kwa kukiuka katiba ya chama chake na
kushiriki maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM
Kamishna wa chama hicho mkoani Kagera Bw Peterson Mushenyera amesema kuwa uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha kamati tendaji ya chama hicho wilaya ya Ngara kilichofanyika juzi
Amesema kuwa Bw Festo amesimamishwa kwa muda wa siku 14 kutokana na kuvunja katiba ya chama chake na kuhudhuria maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika February 5 katika kata ya Kabanga wilayani Ngara
Bw Mushenyera amesema kuwa Bw Festo pia ameandikiwa barua ya kujieleza kwa kamati ya nidhamu ya chama hicho wilayani Ngara inayoongozwa na mwenyekiti Wyclif Samwel

Amenukuliwa
akisema “Ninasema
tunamsimamisha uenyekiti mpaka kesi yake itakapo kwisha na chama chetu hakina
ushirikiano na chama cha mapinduzi”
Aidha
kamati hiyo ya utendaji ya NCCR-Mageuzi wilayani Ngara imemteua Bw Joseph Bucha
kukaimu nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho wilayani Ngara katika kipindi
alichosimamishwa Bw Festo
No comments:
Post a Comment